Pages

Pages

Thursday, September 17, 2015

Magufuli aiteka Kigoma

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo. PICHA NA MICHUZI JR-KIGOMA.
 Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yake, lakini pia atawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi

Magufuli amewataka Wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.

Monday, September 14, 2015

Kampeni za CCM Zanzibar ni hatari, maelfu wajitokeza kuishangilia

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja kwa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.

Sunday, September 13, 2015

Dkt John Magufuli azidi kuchanja mbuga kuomba kuchaguliwa awe rais wa Tanzania

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili katika uwanja wa  CCM mjini Bariadi kwa ajili ya kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mkoani Simiyu.
 PICHA NA MICHUZI JR-SIMIYU.

 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi.
 Wananchi wa Nanga wilaya ya Itilima wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia
 Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya jana.
 Wananchi wakimsiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufui alipokuwa akiwahutubia mjini Meatu jioni ya jana.Dkt Magufuli leo ametembelea wilaya ya Busega,Bariadi,Itilima pamoja na wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk.Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanhunzi jioni ya leo mjini Meatu mkoani Simiyu,Dkt Magufuli alisema kuwa atakapokuwa Rais atakuwa karibu na wananchi wanyonge na kuwa yeye anatoka katika familia ya watu maskini na anajua nini maana ya umaskini,Alisema anatoka kwenye familia ya wakulima na wafugaji  hivyo anajua nini ambacho anatakiwa kufanya kuboresha maisha ya makundi hayo mawili na kwenye hilo atahakikisha anaweka mazingiza mazuri ya matumizi bora ya ardhi.Alisema Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.
"Nitakuwa upande wenu wananchi wanyonge.Serikali yangu ni marufuku watu wa bodaboda kushikwa na polisi.Serikali yangu haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo.Hivyo sitakuwa tayari kuona mama ntile wanatozwa kodi.Najua nitaimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yangu lakini nitawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi,"alisema Dk.Magufuli.
Aliwataka wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Dk.Magafuli aliweka wazi anapenda mabadiliko yenye tija na kwamba Serikali yake itasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma ili wafanye kazi ya kuwatumikia waanchi usiku na mchana na ndio maana atawalipa vizuri na kuongeza hapendi watu wavivu kwenye kazi.

 Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya jana.

 Wananchi wa Mwanhunzi mjini Meatu wakifautilia mkutano huo wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge na Madiwani kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni  Mwanhunzi,mjini Meatu jana jioni Simiyu.
 Wakazi wa Lamadi ndani ndani ya wilaya ya Busega,Mkoani Simiyu wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini humo jana.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Busega,Raphael Chegeni akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
 Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa Busega,mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.Dkt Magufuli aliwaomba wananchi hao kuitunza amani waliyonayo na kuwa kuwapuuza wale wote wenye maneno ya kuleta ufarakanishi katika nchi yetu
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkula,alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi hao akielekea Wilayani Busega kwenye mkutano wa hadhara.
 Maandalizi ya kumpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ndani ya uwanja wa CCM mjini Bariadi yalikuwa kama hivyo pichani.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mwanhunzi,alipomaliza kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo mjini Mwanhunzi,Wilayani Meatu mkoani Simiyu.

Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu yapamba moto, vifaa vya kupigia kura vyakaguliwa

Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka akimpatia maelekezo juu ya NEC inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo alipoitembelea kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
Vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vilivyowasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.

Friday, September 11, 2015

Timu ya Kamati ya viongozi wa dini wajifua

 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum (wa tatu kushoto) na wenzake wakichezea mpira kujaribu viwango vya mipira hiyo baada ya kukabidhiwa na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (wa pili kulia), wakati wa mazoezi ya timu ya Kamati ya Amani inayoundwa na Viongozi wa Dini. Mazoezi hayo yalifanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, sambamba na timu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zaoTanzania,kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wakirafiki kati yao unaotarajia kuchezwa hivi karibuni. Picha na www.sufianimafoto.com
 Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) akimkabidhi mpira Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, Skei Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Alhad Mussa Salum, baada ya mazoezi ya timu hiyo na timu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Nchini, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini leo asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki unaotarajia kuchezwa hivi karibuni.

Bondia Said Mbdelwa kuvaana na Dimoso Septemba 26

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Said Mbelwa anatarajia kupanda uringoni kwa mara nyingine tena kungombania mkanda wa taifa wa chama cha ngumi za kulipwa PST dhidi ya bondia George Dimoso mpambano utakaofanyika Septemba 26 katika ukumbi wa Butihama Villa Club uliopo chanika. 

Mpambano huo wa raundi kumi ulioratibiwa na 
Kocha wa kimataifa nchini Rajabu Mhamila 'Super D' utakuwa ni wa kumaliza ubishi baada ya mpambano wa kwanza Dimoso kudundwa kwa point
Super D aliongeza kuwa siku iyo pia kutakuwa na mipambano mingine mikali itakayowakutanisha mabondia mbalimbali nchini ambapo 
bondia Seleman Zugo atapambana na Abdallah Ruwanje na Adam Ngange atakabiliana na Shabani Mtengela na Said Uwezo atapambana na Hassan Mgosi uku Hamza,

Mchanjo ataoneshana kazi na Ally Maiyo mipambano yote ya utangulizi ni ya raindi sita
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

UNESCO yakabidhi kitabu cha mafunzo ya TEHAMA nchini

IMG_8554
Mkuu wa Ofisi  na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa sekta ya elimu wakati wa hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi  wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katikati ni mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome. Kushoto ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.(Picha zote na Zainul Mzige

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limekabidhi rasmi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakuf unzi  wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es salaam katika hafla iliyohudhuriwa na wadau walioshiriki katika uandazi wa kitabu hicho, ikiwamo serikali ya China.

Kitabu hicho ni matokea ya mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia Serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia. Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama  na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza. Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
IMG_8742
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome wakati wa hafla ya kukabidhiwa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa ajili ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kilichoandaliwa na mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China.

Akipokea kitabu hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome, Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa ameishukuru UNESCO na serikali ya China ya kuwezesha upitiaji wa kitabu hicho kinachotoa mwelekeo wa mafunzo ili kuambatana na maagizo ya viwango yaliyotolewa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),

Thursday, September 10, 2015

Wasanii wa Mabadiliko wafanya yao mkoani Mtwara

Msanii Walter Chilambo akiimba katika Tamasha la Wasanii wa Mabadiliko lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Mtwara. Lengo la Tamasha hilo ni kuwahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 25, 2015.
Msanii Mkoloni akiimba katika Tamasha la Wasanii wa Mabadiliko lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Mtwara. Lengo la Tamasha hilo ni kuwahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 25, 2015.

Tuesday, September 08, 2015

Dkt Bilal afungua mkutano wa Waganga wakuu wa Mikoa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.   Picha na OMR

Ofisi ya Takwimu yatoa neno kuhusu mfumuko wa bei

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015. Kulia ni Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Flaviana Matata ateuliwa kuwa Balozi wa hiyari wa Utalii Tanzania.

flavy   Dr Adelhelm James Meru akimkabidhi Flaviana Matata barua ya kuchaguliwa kwake huku kaimu Mkurugenzi Devota Mdachi akishuhudia, katika ofisi za wizara hiyoFlaviana matata  
Mwanamitindo wa Kimataifa anaefanyia kazi zake za nchini Marekani Flaviana Matata amechagulia na Wizara ya Maliasili kuwa Balozi wa Hiyari 'Good Will Ambassador' kwa kipindi cha miaka mitatu kwa dhumuni la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.
Flaviana ambaye juzi alikuwa mmoja kati ya shuhuda wa kushuhudia wizara ya maliasili na utalii wakizindua rasmi tangazo litakalokuwa linatangaza vivutio vya Tanzania nje ya anchi alitawazwa leo hii na katibu mkuu Dr Adelhelm James Meru aliyemkabidhi kwa niaba ya Waziri , Mheshimiwa Lazaro Nyalandu huku Kaimu Mkurugenzi Madam Devota Mdachi akishuhudia.
 

Bayport yazindua huduma ya Jibayportphonishe

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, kushoto, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya simu za mikononi aina ya Huawei ijulikanayo kama 'Jibayportphonishe', uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Micka Mavoa, Mkurugenzi wa Cape View, Kampuni inayoshirikiana na Bayport katika huduma hiyo ambayo mteja akikopa simu atapelekewa hadi mahala anapohitaji ifike. Picha na Mpiga Picha Wetu.                  
                                                                                               

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, imezindua huduma yake mpya ya kukopesha (Smartphone) simu za mikononi aina ya Huawei zenye thamani ya Sh 140,000, ikiwa na lengo la kuwawezesha Watanzania ambao ni watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa kumiliki simu wakati wowote ili ziwakwamuwe katika suala zima la mawasiliano ya simu za mikononi, huduma inayotambulika kama 'Jibayportphonishe'.

Kuanzishwa kwa huduma hiyo ya mikopo ya simu za mikononi kumekuja siku chache baada ya taasisi hiyo pia kuzindua huduma ya bima ya magari, pikipiki na bajaj, ambapo zote kwa pamoja ni mkombozi kwa Watanzania, wakiwamo wale wenye kipato cha chini na cha kati.

 Ngula Cheyo akizungumza jambo, kulia ni Micka Mavoa, Mkurugenzi wa Cape View

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba kuanzishwa kwa huduma hiyo kutaifanya jamii iwe katika kiwango kizuri cha mawasiliano, hivyo kukuza pia uchumi wao.

Alisema kwamba badala ya mtumishi wa umma na wale wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa kuwekeza kidogo kidogo ili wanunuwe simu watakazo, sasa wanaweza kukopeshwa simu hizo na kupelekewa hadi katika maeneo yao wanayopatikana.
Alisema simu hizo zitaambatana na ofa ya intaneti MB 500 bure kila mwezi kwa miezi sita kutoka katika Kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania, huku mteja akilazimika kulipa Sh 9000 kila mwezi, katika kipindi cha miezi  24.

Thursday, September 03, 2015

Watoto watatu wafutwa machozi na bima ya elimu ya Bayport Biharamulo

Na Mwandishi Wetu, Kagera
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, jana imewakabidhi hundi ya Sh Milioni tatu watoto watatu wilayani Biharamulo, mkoani Kagera, kwa ajili ya kunufaika na huduma ya Bima ya Elimu iliyoachwa na mzee wao Karume Ochieng aliyefariki Dunia, huku akiwa amejiunga na huduma ya bima kwa ajili ya watoto wake hao.
Mratibu Mauzo wa Bima ya Elimu wa Taasisi ya Kifedha inayotoa Mikopo(Bayport Financial Services, Ruth Bura akikabidhi mfano wa hundi kwa familia ya marehemu Karume  ambaye alikuwa amejiunga na bima hiyo katika shule ya msingi Nyamuhuna iliyopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera, kushoto ni Meneja Mauzo wa  Bayport Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Taasisi hiyo imeanzisha bima ya elimu ili kusaidia kiasi cha ada kwa watu wa karibu walioainishwa na mteja wao endapo atakumbwa na umauti.


Watoto hao ambao wamepewa hundi hiyo itakayowawezesha kila mwaka katika vipindi vya miaka mitatu mfululizo kupewa Sh Milioni moja kwa ajili ya kuwalipia ada katika shule wanazosoma ni pamoja na Athieno Karume, Chacha Karume na Aaptalius Karume.

Makabidhiano ya hundi kwa familia ya marehemu Karume yakiendelea wilayani Biharamulo, mkoani Kagera.

Akizungumza katika makabidhiano ya hundi hiyo kwa watoto hao, Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema kwamba kukabidhi hundi hiyo kutawafanya watoto hao wasome kwa raha, baada ya kuwekewa bima hiyo na marehemu baba yao kutokana na mapenzi mema na vijana hao wanaoendelea na masomo.

Wednesday, September 02, 2015

Chama cha Ukombozi Chauma chazindua kampeni zake Jijini Dar es Salaam


 Mwananchi aliyevalia nguo za Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiondolewa na askari polisi baada ya kujipenyeza kwenye uzinduzi wa kampeni za Chama cha Ukombozi Umma (Chauma), uliofanyika viwanja vya Bakhresa Manzese Dar es Salaam leo.
 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi (Chauma), Dk. Hashim Rungwe, akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika viwanja vya Bakhresa Manzese Dar es Salaam leo.
 Mzee wa chama hicho, Mbwana Hassan Mbwana akihutubia kwenye uzinduzi huo.

Serikali ya Magufuli kufanyia kazi migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji kwa kupima ardhi yote ya vijijini

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama hicho. Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa amepokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama.

Na Joachim Mushi, Dodoma
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu amesema Serikali itakayoundwa na chama hicho endapo itashika dola katika Uchaguzi Okuu wa Oktoba, 2015 itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi. Bi. Suluhu ametoa kauli hiyo alipokuwa akinadi ilaya ya CCM katika Majimbo mawili tofauti ya Kongwa na Chilonwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya kampeni kuwashawishi Watanzania waweze kuipa ridhaa tena Chama Cha Mapinduzi ili kiunde Serikali na kuwatyumikia wananchi.
 Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.

Wwanamuziki wa Tanzania waanza kupata huduma ya bima ya afya


Mwaka 2004, John Kitime ambaye kwa sasa ndie Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (Tanzania Musicians Network-TAMUNET) alihudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Muziki Duniani –International Federation of Musician (FIM). Katika mkutano huo moja ya maazimio ya mkutano ule ilikuwa kila nchi ihakikishe inaanzisha utaratibu wa Bima ya Afya kwa wanamuziki wake. 

Mara baada ya kurudi Tanzania, kwa kushirikiana na viongozi wengine wa TAMUNET, Kitime alianza kufuatilia uwezekano wa kupata huduma ya Bima hiyo kwa wanamuziki. Kwa bahati mbaya hakukuwa na njia yenye gharama nafuu ya malipo ya BIma hiyo ambayo mwanamuziki wa kawaida angeweza kuyamudu. Kulikuweko na kampuni ambayo iliweza kutoa huduma hiyo kwa gharama ya dola 300 kwa mwaka kwa mwanamuziki mmoja. 
Wasanii katika semina kuhusu BIma Ya Afya iliyofanyika BASATA karibuni
Kampuni nyingine za Bima zilizotembelewa hazikuonyesha ushirikiano katika jambo hilo. TAMUNET iliwasiliana pia na mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa katika kipindi hico mfuko ulikuwa hauna mamlaka ya kuhudumia watu waliokuwa nje ya ajira ya serikali na mashirika ya umma. TAMUNET iliwasiliana na Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye alishauri TAMUNET kuwasiliana na NGO moja ambayo ilikuwa na makao yake makuu Sinza, na kweli NGO hiyo ilikubali kuwa ingeweza kutoa huduma ya Bima ya Afya kwa wanamuziki kwa gharama ya shilingi 3000/- tu kwa mwezi, lakini huduma hii ilikuwa ni kwa hospitali kadhaa tu jijini Dar es Salaam.

Mahakama ya Mwanzo ya Mbagala yasema ndoa ya Thadei Mtembei na Magreth Mwangu ni batili

court_gavel
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Mbagala, Dar es Salaam imesema haiwezi kumuamuru Mmiliki wa nne za Shule za Sekondari, St Mathew na St Marks ,Thadei Mtembei kutoa talaka kwa Magreth Mwangu kutokana na ndoa yao kuwa batili. Akisoma hukumu hiyo leo, Hakimu Rajab Tamambele alisema ndoa aliyofunga Mwangu pamoja na Mtembei ambayo ni ya kimila ni batili kwa kuwa mdai hakutoa cheti cha ndoa hiyo ilipofungwa.

Alisema kwa misingi hiyo, mahakama haiwezi kumuamuru Mtembei kutoa talaka kwani aliwasilisha cheti cha ndoa ya mke mmoja aliyoifunga mwaka 1985.
pia alisema mahakama hiyo haiwezi kugawa mali kama ambavyo mdai ameiomba mahakama, ambapo amesisitiza kuwa mgawanyo wa mali unatokana na ndoa halali ambayo baba na mama wanaishi pamoja. ‘’Mashahidi wote wameeleza kuwa Mtembei na Mwangu walikuwa wanakutana hoteli ya Sleep Inn. Kwa hivyo mahakama inaona kuwa uhusiano kati ya mdai na mdaiwa ulikuwa wa kimapenzi pekee au hawara na kwa lugha ya kistaarabu tunaita mzazi mwenzie,’’ aliongeza Tamambele.