Pages

Pages

Monday, August 24, 2015

Bodaboda Kipunguni B waanzisha Ligi ya kujenga afya zao kwa kupitia michezo

Madereva bodaboda wa mtaa wa Kipunguni 'B' kata ya Kivule Manispaa ya Ilala wameanzisha ligi  ya mpira wa miguu kwa ajiri ya kuendeleza kujenga afya zao kwa michezo kwani michezo ni afya kwa wote, wakati wa ufunguzi huo wa ligi hiyo ya madereva bodaboda wadhamini wa ligi hiyo ambao ni Mfuko wa pensheni wa (PSPF)nao hawakuwa mbali kwaajiri ya kuwawezesha madereva hao kwa kipindi chote cha ligi hiyo.

 
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza na madereva bodaboda wa Kipunguni 'B' kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi hiyo mgeni rasmi ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam Josephat Sylvery Tirumanywa amewaasa madereva hao kuwa waweze kucheza kwa amani michezo yote na pia waweze kuwa ni miongoni mwa watu watakao jiunga na na mfuko wa (PSPF) ka kupitia (PSS) kwaajiri ya kuendelea kupata huduma zilizo bora na  zenye uhakika .

Pia Afisa masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Ismail Juma amesema wameamua kuungana na madeeva boda boda hao ili kuweza kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na kufaidika na mafao mbalimbali yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga na mfuko huo wataona matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao wanategemewa na familia zao hivyo kama Pspf wana mafao ambayo wataweza kujikwamua kama mafao ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la uzazi hata fau la nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala hauto jutia 
Naye Bw.Delphin Richard ambaye pia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) amewasisitiza madereva kutii sheria za barabarani na pia kuweza kucheza ligi hiyo kwa amani maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na upendo ,hivyo kati ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya kazi kwa umoja na hivyo kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi yetu inajengwa na sisi watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi tuwapo barabarani,aliongeza kwa kuwapa shukrani madereva ya kuweza kuchagua mfuko wa pensheni wa Pspf kuwa wadhamini wa michuano hiyo kwani PSPF ipo kwaajiri ya kila mmoja  na kuweza kuwaasa  waweze kuwahamasisha watu mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha mabadiliko ya wananchi mbalimbali yanatokea kimaisha ,elimu,afya na mengine mengi.

Mfuko wa pensheni wa PSPF unafuraha ya kuwa kwa sasa wananchi wanajua kile kilicho sahihi nakuongeza kuwa wananchi mbalimbali waweze kufika maeneo ya kipunguni B ilikuweza kushirikiana na madereva hao kwa kuwashangilia wakati ligi ikiwa inaendelea na ligi hiyo itakayo dumu kwa takibani wiki moja.


No comments:

Post a Comment