Pages

Pages

Tuesday, August 18, 2015

Bayport yaanzisha huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj

Mratibu wa Bima kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, katikati akizungumza katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na Bajaj kwa kushirikiana na Kampuni ya NIKO Insurance. Kulia ni  Meneja Uendelezaji wa Biashara wa  NIKO Insurance, Jabir Kigoda na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Niko, Mannaseh Kawoloka.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, imezindua huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj, ikiwa na lengo la kurahisisha masuala ya usafiri kwa wateja wao ili kukwamua zaidi. Kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kumetajwa kuwa kutachangia kwa kiasi kikubwa wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri waliokuwa wakishindwa kulipa bima kwa wakati na wakati mwingine mteja kupata ajali hali ya kuwa hana huduma ya bima inayoweza kumlinda.
Oparesheni Meneja wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, kushoto akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na bajaj. Anayefuata ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka.
Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka katikati akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj inayoendeshwa na Taasisi ya Bayport Financial Services. Kulia kwake ni Mratibu wa bima hiyo, Ruth Buran a kushoto kwake ni Meneja Oparesheni wa Bayport, Charles Mgeta. Picha zote na Mpiga Picha Wetu. 
Wakati shughuli ya uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj kutoka Bayport Financial Services kwa kushirikiana na NIKO Insurance ukiendelea Makao Makuu ya Bayport leo asubuhi.
Meneja Madai wa Niko Insurance, David Mshuza, akiafuatiwa na Cecilia Peter na Lester Chinyang'anya. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Akizungumza leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima hiyo kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema huduma yao wanayoshirikiana na NIKO Insurance ina lengo kubwa la kumrudisha mteja wao (mkata bima), katika hali aliyokuwa nayo kabla ya kupata ajali hiyo.

Alisema mara kadhaa baadhi ya Watanzania wamekuwa wakikimbizana na askari wa usalama barabarani kwa sababu hawana bima kwenye vyombo vyao vya usafiri, ila kwa kupitia huduma yao mpya, sasa kila mtu anaweza kujiunga na bima kwa njia rahisi, wakiamini kuwa ni sehemu yao ya kuhakikisha wateja wao wanakuwa kwenye usalama ili watimize wajibu wao kufanya kazi na kukuza uchumi wao na wa Tanzania kwa ujumla.
“Ili mtu aweze kujiunga na huduma yetu ya Bima kutoka Bayport Financial Services, kwanza anatakiwa kujaza fomu yetu ya mkopo na ile fomu ya udhibitisho wa bima, bila kusahau nyaraka za umiliki wa gari lake ili tujiridhishe na umiliki wake.


“Baada ya hapo, gari lake litapigwa picha tano kila pembe, ikiwa ni nyuma na mbele na kwenye injini na tukimaliza hatua hiyo, mteja wetu atapatiwa mkataba wa bima pamoja na ‘sticker’ kuonyesha kuwa yupo kwenye bima, huku huduma hiyo ikiwa ni rahisi kwa sababu gharama za bima kwa mwaka ni kuanzia Sh 354,000 pamoja na VAT,” Alisema.


“NIKO tunajisikia faraja kubwa kushirikiana na wenzetu Bayport Financial  Services kutoa huduma bora na kiwango cha juu, hususan kwa kupitia huduma hii mpya ya bima ya magari, tukiamini kuwa itawafanya Watanzania wote watembee kifua mbele, maana ile presha ya kukimbiana na watu wa usalama barabarani itakuwa imepatiwa ufumbuzi,” alisema Kigoda.


Bayport Financial Services ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma mbalimbali za mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa, bila kusahau mradi wa mikopo ya viwanja vya Vikuruti unaoendelea na kuwafanya Watanzania watembee kifua mbele, huku taasisi hiyo ikifanikiwa kuwa na matawi 80 Tanzania Bara, hivyo kutoa huduma bora na kwa njia rahisi kwa kupitia matawi yao au mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz.



Naye Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda, alisema kuwa huduma hiyo ni nzuri na rahisi inayoweza kuwanufaisha wateja na Watanzania wote, hivyo wanapaswa kuichangamkia ili kuwaweka katika usalama wao na wa vyombo vyao vya usafiri.


No comments:

Post a Comment