Pages

Pages

Friday, June 05, 2015

Watanzania wavichangamkia viwanja vya Bayport Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATANZANIA wameendelea kuvichangamkia viwanja vya mkopo vinavyotolewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
 Hawa ni miongoni mwa Watanzania waliohamasika kutembelea katika viwanja vilivyokuwa kwenye mradi wa Vikuruti kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ambavyo vinatolewa kwa wananchi kwa mkopo. Wakopaji ni watumishi wa umma, kampuni binafsi na wajasiriamali.
Eneo la viwanja vya Vikuruti vinavyoonekana huku barabara ikionekana pichani.
Kuchangamkiwa kwa viwanja hivyo kumekuja siku chache baada ya kuzindua huduma mpya ya mikopo ya viwanja hivyo kutoka Bayport, ikiwa ni ishara nzuri na njia ya kuwapa fursa Watanzania ya kumiliki nyumba.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema watu wengi wamekuwa wakituma maombi ya kuomba kupewa viwanja hivyo, tangu huduma hiyo ilipozinduliwa rasmi.

Alisema kwamba baadhi ya watu walioonyesha nia ya kuvipata viwanja hivyo pamoja na kutuma maombi yao, pia wamekuwa wakitembelea eneo kulipokuwa na viwanja hivyo ili wajiridhishe kwa ajili ya kujipatia viwanja hivyo vinavyokopeshwa kwa minajiri ya kuwakwamua Watanzania, ukizingatia kuwa ardhi inapanda thamani siku hadi siku.

“Jana (juzi) zaidi ya watu 82 wamekwenda Vikuruti, Kibaha kujionea eneo lenyewe na kuchagua viwanja wapendavyo, ikiwa ni mwendelezo mkubwa wa wananchi wanaotuma maombi ya kukopa viwanja vya Bayport, wakichukua fomu bure z  kwa kupitia matawi yetu yaliyoenea nchi nzima, bila kusahau kwenye matawi ya Bank of Afrika (BOA).

“Huduma hii ni murua kwa Watanzania wote, tukiamini kuwa ni sehemu ya kuwapatia wananchi urahisi wa kumiliki vitu vyenye thamani ikiwamo ardhi wanayoweza kuitumia kwa mambo mengi, ikiwa nyumba za kuishi na za biashara, huku thamani ya viwanja vikianzia Sh 1,400,000 na kuendelea kwa viwanja vyenye ukubwa tofauti vya kujenga nyumba za kuishi na biashara kama vile shule, vituo vya afya, nyumba za kulala wageni na hoteli,” alisema Cheyo.
Cheyo alisema nafasi ni chache, maana maombi yanafanyika kwa siku (20), kuanzia Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya Bayport Financial Services na matawi ya bank of Africa (BOA), ambapo malipo ya awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport iliyopo BOA.

Kwa mujibu wa Cheyo, fomu ya maombi na nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi BOA au ofisi za taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima na baada ya Juni 10, mteja atatakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka kwenye taasisi yao huku watumishi wa umma na wa kampuni binafsi wakiweza kukopeshwa kiwanja na kukabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90) watakapokamilisha mkopo wao.

No comments:

Post a Comment