Pages

Pages

Thursday, June 25, 2015

Mbunge Nassari amaliza mikutano ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura

Rubani wa Helkopta akimfunga mkanda Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mikutano ya hadhara ya kuhasisha wananchi kujitokeza kujinadikisha katika daftarai la kudumu la wapiga kura.
Wananchi katika kata ya King'ori wakimpokea Mbunge Nassari wakati alipowasili katika mkutano wa hadhara wa uhamasishaji zoezi la uandikishaji .
Kada wa Chadema ,Samwel Nnko akizunumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya King'ori .
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ,akiwa na mtoto aliyevalia fulana iliyoandikwa Dogo Janja jina ambalo Nassari alipewa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliompatia Ubunge,
Mbunge Nassari akiwahutubia wananchi katika kata ya King'ori jimbo la Arumeru Mashariki akihamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Ng'arenanyuki waliofika katika mkutano wa hadhara wa uhamasishaji juu ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura .
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Josgua Nassari akiwahutubia wananchi wa kata ya Ngarenanyuki katika jimbo la Arumeru Mashariki akihimiza kujitokezakwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katia daftari la kudumu la wapiga kura.

Baadhi ya wananchi katika kata ya Ngarenanyuki waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment