Pages

Pages

Saturday, May 09, 2015

World Lung Foundation yazindua mradi wa elimu kwa mtandao kusaidia uokoaji wa akina mama na watoto

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (wapili kulia), akiwa na baadhi ya watendaji wa Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini wakishudia uzinduzi wa mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na shirika hilo katika vituo vya Afya 13.

TAASISI ya World Lung Foundation (WLF) Tanzania imezindua mradi wa elimu kwa njia ya mtandao katika hatua mpya ya kusaidia kuboresha ubora wa huduma za wajawazito pamoja na akina mama na watoto wao. Mradi huu wa  Mawasiliano umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden  (Swedish International Development Cooperation, (Sida)) na Shirika la Merck For Mothers. Mradi huu upo katika vituo vya afya 13 vinavyo fadhiliwa na WLF katika mikoa ya Kigoma, Pwani na Morogoro.


Mfumo huu wa WLF Tanzania wa  elimu kupitia mtandao (e-learning) umeundwa ili kuboresha ujuzi  wa wafanyakazi wa vituo vya afya na kuongeza wao uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika kliniki zitoazo huduma za afya. Mfumo huuutawasaidia  kufanya maamuzi ya kitaalam kuhusu usimamizi wa dalili hatarishi za ujauzito, huduma wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua kwa ajili ya akina mama na watoto wao.Mafunzo haya yatawawezesha watoa huduma ya afya kuwasiliana na kupata taarifa muhimu za kuongeza ujuzi, kusoma Makala za jarida za kitaalam, kuona filamu zinazoelimisha, picha na masomo ya kujifunzia. Wafanyakazi wa afya  pia wanaweza kutumia jumuishi ya vikao vya mitandao na kubadilishana ujuzi na taarifa kuhusu changamoto na mafanikio  yao pamoja na wenzao  na wataalam waandamizi katika vituo vya afya 13.

“Tunaiomba serikali kuharakisha upatikanaji wa mtandao yaani intaneti vijijini ili tuweze kuunganisha vituo vya afya kupitia mkongo wa taifa, ili vituo vingi vya afya viweze kutumia mradi huu kwa njia ya gharama nafuu, "alisema Dk Nguke Mwakatundu, Mkurugenzi  wa Tanzania, World Lung Foundation. "Uwekezaji kama huu unaweza kusaidia kuokoa maisha ya mama wengi zaidi na watoto wao."
Programu hii ya elimu kwa njia ya  mtandao ni maendelezo ya uboreshaji unaofanywa na WLF na sehemu ya mkakati wa matumizi ya miradi wa ICT ili kusaidia kuboresha matokeo ya afya. 
Jamii ya huduma na kujifunza
Vituo 13 vya afya vilivyounganishwa na mfumo huu ni pamoja na Kituo cha Afya cha Kibiti na Hospitali ya Wilaya Utete katika wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani. Katika Mkoa wa Morogoro, vituo vya afya ni pamoja na Kituo cha Afya cha Mlimba kilichopo katika wilaya ya Kilombero , na Mtimbira na Mwaya vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya ya Mahenge Ulanga. Katika mkoa wa Kigoma, vituo vya afya ni pamoja na Kituo cha Afya Nguruka katika wilaya ya Uvinza, Kituo cha Afya cha ujiji na Hospitali ya Mkoa Maweni Kigoma mijini wilaya, Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, Hospitali ya Wilaya ya Kibondo na Mabamba Kituo cha Afya katika Kibondo wilaya na Kakonko Kituo cha Afya katika wilaya ya Kakonko . Pamoja na haya, vituo viwili vyaafya katika mkoa wa Kigoma - Kituo cha Afya cha Buhingu katika wilaya ya Uvinza ya na Kituo cha Afya cha Nyenge katika  wilaya ya Kasulu – wataunganishwa na mpango huu mbunifu wakati marekebisho ya  kiufundi yatakapokamilika.

No comments:

Post a Comment