Pages

Pages

Sunday, May 10, 2015

Ratiba ya vikao vya ndani vya CCM yatolewa, kuanza Mei 18

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake wa Uenezi Ndugu Nape Nnauye kimetangaza ratiba za Vikao vya juu vya Chama hicho kuanzia tarehe 18 mpaka 23 Mjini Dodoma.
Tarehe 18 mpaka 19 Mei Kikao Cha Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana

Tarehe 20 Mei kutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Ndg Jakaya Kikwete.

Tarehe 21 mpaka 22 kutakuwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Ndg Jakaya Kikwete.

Vikao hivyo ambavyo vitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makao Makuu 
Dodoma maarufu kama "whitehouse" vinategemea kujadili ajenda zifuatazo.

1. Kuwasilisha na kujadili ripoti ya hali ya siasa nchini.
2. Ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge, urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Kupitia Rasimu ya Kwanza ya maboresho ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020.
4. Mapendekezo ya uboreshaji wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.
5. Namna ya Ushiriki na Mkakati wa Ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment