Pages

Pages

Thursday, April 09, 2015

Watatu wa Dar es Salaam, Songea na Bukoba wajishindia mamilioni kutoka Bayport Financial Services

Meneja Utawala wa Bayport Financial Services aliyezibwa macho, Evalyine Hall, akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, inayoendeshwa na taasisi hiyo ambapo washindi watatu ambao ni Hyasint Mbunda (Songea), Phaustine Mbilinyi (Dar es Salaam) na Allen Bishubo (Bukoba), walipatikana na kila mmoja kushinda Sh Milioni moja. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo na kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein. Picha na Mpiga Picha Wetu.
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WASHINDI watatu waliokopa fedha kwa njia ya Mtandao wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wamejishindia Sh Milioni moja kila mmoja, kutokana na shindano hilo lililoanzishwa maalum kwa ajili ya wateja wao waliomua kuutumia mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz kupata huduma mbalimbali.

Washindi hao wamepatikana kutoka kwenye droo ya mwezi wa Aprili, iliyoendeshwa na Bayport Financial Services kwa kusimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Meneja Utawala wa Bayport Financial Services Evelyine Hall katikati akisoma koponi ya mmoja wa washindi wa Kopa Bayport kwa njia ya Mtandao inayoondeshwa na taasisi hiyo ya kifedha. Kulia kwake ni Msimamizi wa Michezo ya Kubatisha Tanzania, Humud Abdulhussein na kushoto ni Ngula Cheyo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba washindi hao watatu wamepatikana baada ya kuamua kukopa kwa njia ya mtandao wao waliyouzindua mwezi uliopita.
Ngula Cheyo (katikati) ambaye ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services akizungumza jambo katika droo ya kutafutwa washindi watatu wa bahati nasibu inayoandaliwa na taasisi hiyo ambao kila mmoja alishinda Sh Milioni moja.

“Tuliamua kuanzisha huduma ya kukopa kwa njia ya mitandao tukiamini ni huduma rahisi inayoweza kuwafanya Watanzania wote wafurahie kwa pamoja na kukuza uchumi wetu, hivyo tukaona tufike mbali zaidi kwa kuchezesha droo yetu ya kuwapatia Sh Milioni moja washindi watatu kila mwezi.
Ngula Cheyo (katikati) ambaye ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services akizungumza jambo katika droo ya kutafutwa washindi watatu wa bahati nasibu inayoandaliwa na taasisi hiyo ambao kila mmoja alishinda Sh Milioni moja. Kulia ni Humud Abdulhussein kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha na kushoto ni Meneja Utawala wa Bayport Financial Services, Evalyine Hall.
Shughuli ya kutafutwa washindi wa Kopa na Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz inaendelea.
Jamani huyu ndiye mshindi. Ndivyo anavyoenekana kusema Meneja Utawala wa Bayport Financial Services katika droo ya kutafutwa washindi watatu waliokopa kwa njia ya mtandao.

Washindi hao ni Phaustine Mbilinyi (Dar es Salaam), Hyasint Mbunda (Songea) na Allen Bishubo (Bukoba)ambao kila mmoja amejinyakulia Sh Milioni moja baada ya kushinda katika bahati nasibu yetu hii, huku tukiamini kuwa wateja wengine wanao uwezo wa kushinda katika droo nyingine ijayo, ukizingatia kuwa Bayport ipo kwa ajili yao katika kutoa huduma bora zinazoweza kuwakwamua, ikiwamo ya mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana,” alisema Cheyo.

Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka kwenye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein alisema washindi hao baada ya kupatikana walipigiwa simu ili wataarifiwe ushindi wao na jinsi ya kupata zawadi zao za Sh Milioni moja kila mmoja.

“Huduma ya kukopa kwa njia ya mtandao inayoendeshwa na Bayport Financial Services ni nzuri na rahisi, ambapo pia ipo fursa ya kushinda pesa taslimu kwa wale watakaoamua kukopa kwa njia hiyo,” alisema.

Bayport Financial Services ni taasisi ya kifedha inayoongoza kutoa mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na taasisi hiyo.


No comments:

Post a Comment