Pages

Pages

Monday, April 06, 2015

Mwenyekiti wa NRA Taifa kuzikwa leo saa saba mchana makaburi ya Nzasa Kilungule, Mbagala Charambe, jijini Dar es Salaam

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA), Rashid Mtuta, anatarajiwa kuzikwa leo saa 7 mchana katika makaburi ya Nzasa Kilungule, yaliyopo Mbagala Charambe, ambapo ndio nyumbani kwake.

Katika mazishi hayo, watu mbalimbali wanatarajiwa kushiriki katika tukio hilo, akiwamo Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Mheshimiwa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.

Naibu Katibu Mkuu wa NRA Taifa, Hassan Kisabya, aliumbia mtandao huu kuwa tararatibu za mazishi zimeshaandaliwa, wakiwamo ujio wa wageni katika maziko ya mwenyekiti wao.

“Bado NRA hatuamini kwamba mwenyekiti wetu ametuacha katika wakati mgumu wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, hata hivyo badala ya kulalamika sana na kumkufuru Mungu, tunamuombea.

“Nilkuwa kimya bila kupata neno la kueleza katika msiba huu mzito kwetu, ukizingatia kuwa huu ni mwaka mgumu kwetu kutokana na chama kuwa na shughuli ngumu ya Uchaguzi Mkuu,” alisema Kisabya.

Mbali na kuwa Mwenyekiti wa NRA, Mheshimwa Mtuta pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Siasa ya Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania.

No comments:

Post a Comment