Pages

Pages

Sunday, March 22, 2015

Zitto ajiunga rasmi na ACT, leo kuwatangazia wananchi kupitia waandishi wa habari leo saa tano

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ALIYEKUWA Mbunge Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Zitto Kabwe, amejiunga rasmi kwenye Chama chake kipya kinachojulikana kama Alliance for Change and Transparency ( ACT), imefahamika.
Zitto Kabwe kushoto baada ya kusaini kujiunga rasmi kwenye chama cha ACT usiku wa kuamkia leo, jjini Dar es Salaam. Picha kwa hisani yaa mitandao.

Habari zlizoanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kwa mtu wa karibu zilisema tamko la kuhamia kwenye chama hicho kipya atazitoa leo saa tano asubuhi, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kabla ya kukutana na waandishi wa habari, tayari picha zake zimeanza kuzagaa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha wakati anasaini juu ya kujiunga kwenye chama hicho kinachotarajia kuingia kwenye Uchaguzi wa ndani hivi karibuni.

Duru za siasa zinasema endapo Zitto asingeweza kujiunga na chama hicho kipya jana, basi asingekuwa na sifa ya kugombea uongozi wowote ndani ya ACT, inayotaka mwanachama wake aliyejiunga siku saba kabla ya uchaguzi wao.

Hata hivyo juu ya mwelekeo wake kisiasa na namna gani anaweza kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa mambo mbalimbali, Zitto ataongea mengi katikaa mkutano huo na waandishi wa habari, ikiwa ni siku moja baada ya kuachia ngazi rasmi kwa kuaga bungeni.

No comments:

Post a Comment