Pages

Pages

Tuesday, March 10, 2015

Wateja wa Bayport watakaokopa kwa njia ya mtandao online kushindania Milioni 1

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATEJA wa taasisi ya Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mambo ya mikopo wanaweza kujishindia jumla ya Sh Milioni moja, endapo wataamua kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, uliozinduliwa rasmi jana, jijini Dar es Salaam.
 Msimamizi wa michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Milao kulia akipata  maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya mtandao Online) wa Bayport Financial Services, Zainabu Kalufya, katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao kwa www.kopabayport.co.tz, uzinduzi uliofanyika leo Makao Makuu ya Bayport, jijini Dar es Salaam. Mteja atakayekopa kwa njia ya mtandao anaweza kushinda Sh Milioni moja. Picha kwa Hisani ya Bayport.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema kwamba kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya na ya haraka ni sehemu ya kuwapatia wateja wao na Watanzania kwa ujumla huduma bora na za kiwango cha juu.
Alisema uzinduzi wao wa huduma ya kukopa kwa mtandao (online), utawawezesha kwa kiasi kikubwa wateja wao kushinda Sh Milioni Moja, baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kumtafuta mshindi.

“Sasa mtu anaweza kukopa kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi endapo atakopa kwa njia ya internet, huku akiweza kujishindia Sh Milioni kutoka Bayport Financial Services.
“Naamini sasa wateja wetu wataendelea kufurahia huduma nzuri kutoka kwetu kwa ajili ya kurahisisha maisha, ukizingatia kuwa mikopo ya Bayport haina dhamana wala amana,” alisema.

Naye Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao, alisema kwamba mfumo wa ukopaji kwa njia ya mtandao ya Bayport ni rahisi na nzuri, hivyo kila mtu anaweza kukopa na kujishindia zawadi hiyo ya Sh Milioni moja.

“Kila mtu anaweza kukopa na kushinda kutokana na mfumo uliokuwapo kuwa rahisi, maana mteja anaweza kutumia njia mbalimbali zenye mtandao kama vile kompyuta na simu za mikononi ambapo baada ya kutuma maombi, yatapokewa kwa haraka na wahudumu wao,’ alisema Millao.

Bayport ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ambapo imefanikiwa kufungua ofisi katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania ili kuwafikishia karibu huduma zao.

No comments:

Post a Comment