Pages

Pages

Thursday, March 19, 2015

Rais Jakaya Kikwete atua Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, pia kuhutubia EAC

Na Mwandishi Wetu, Burundi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya Jumatano, Machi 18, 2015 amewasili nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Maua kutoka kwa watoto waliokuja kumlaki katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bujumbura ambapo alianza ziara ya kikazi ya siku mbili.
 Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bujumbura leo jioni.Rais Kikwete yupo nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mji mkuu wa Burundi wa Bujumbura, Rais Kikwete amepokelewa na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza na pamoja na mamia kwa mamia ya wananchi wa Burundi. 
Rais Kikwete ambaye amewasili Burundi akitokea Dodoma ambako alikuwa katika ziara ya kikazi pia leo Machi 19, 2015, atahutubia Bunge la Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki (EALA) katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) katika hotuba ya The State of the East African Community Address.

Saa chache baada ya kuwasili Bujumbura, Rais Kikwete amehudhuria chakula cha jioni ambacho ameandaliwa na Rais Nkurunzinza kwenye Hoteli ya Panoramique. 

Wabunge wa Bunge la EALA pia wamehudhuria chakula hicho cha jioni.Rais Kikwete ataondoka Burundi mara baada ya kuhutubia EALA kurejea mjini Dodoma kuendelea na ziara yake.


 Rais Kikwete na mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipokea heshima wakati nyimbo za Taifa za nchi zao zikipigwa
 Rais Kikwete na mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakikagua gwaride liloandaliwa na jeshi la Burundi.
Rais Kikwete akiwa na Mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi jijini Bujumbura jana  jioni. 
Picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment