Pages

Pages

Wednesday, March 18, 2015

Mbunge alia na unyanyapaa kwa walemavu wa ngozi

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Al-Shaymaa Kwegyir, akizungumza na wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki hawapo pichanai, katika kongamano la kujadili nini kifanyike kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) lililofanyika jana chuoni hapo. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Keto Mshigeni na Kulia ni Kokushubika Kairuki. 
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Viti Maalum ambaye pia ni mlemavu wa ngozi (albino),  Al -Shaimaa Kweigyir, amekemea vikali unyanyapaa unaofanywa na baadhi ya Watanzania juu ya jamii yenye ulemavu wa ngozi na kusema kwamba inawafanya watu hao waishi kwa unyonge.

Mbunge huyo aliyasema hayo jana katika kongamano la kujadili nini kifanyike ili kutokomeza mauaji na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa walemavu wa ngozi llilofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wanazuoni.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Al-Shaymaa Kwegyir, katikati akiwa kwenye kongamano la wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki kujadili nini kifanyike kutokomeza mauaji ya albino. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Keto Mshigeni na Kulia ni Kokushubika Kairuki.

Akizungumzia unyanyapaa huo, Shaimar alisema kwamba bado baadhi ya wana jamii wamekuwa wakiendeleza vitendo vya unyanyapaa vinavyofanywa na watu ambao wamekuwa na mtizamo hasi juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Alisema kwamba jamii ikielimika na kutambua haki sawa kama walivyokuwa nazo wao juu ya ndugu zao albino, hata mauaji yatapungua kama sio kwisha kabisa, hususan kwa kuhakikisha kwamba wanawalinda na kuwathamini wakati wote.
 Mbunge wa Viti Maalum CCM, AL Shaimaa Kweigyir kushoto akizungumza na Kokushubika Kairuki katika kongamano hilo lililohudhuriwa na watu mbalimbali.
 Baadhi ya wahudhuriaji wa kongamano hilo wakisikiliza mada zilizokuwa zinazungumzwa.
Watu wanasikiliza kwa makini katika kongamano hilo la kujadili juu ya mauaji ya albino yanayoendelea kutokea hapa nchini.

“Wapo watoto wanaozaliwa katika hali ya albino ambao wamekuwa wakiishi kwa mashaka makubwa kutokana na unyanyapaa dhidi ya jamii nyingine ambayo ukiangalia kwa kina hakuna tofauti yoyote kati ya albino na wengineo.

“Naomba jamii ione albino ni watu kama wao kwa kuhakikisha kwamba wanawathamini, wanawajali na kuwalinda wakati wote, huku wakianzia kwenye uondoaji wa fikra mgando na unyanyapaa wanaofanya kwa baadhi ya kaya,” alisema.

 Mbunge Shaimar ni miongoni mwa viongoz wa serikali waliojiweka busy katika kutafuta mbinu za kuweza kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino yanayoendelea kutokea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment