Pages

Pages

Monday, March 02, 2015

Mama wa Katibu wa Mbunge afariki Dunia wilayani Kibaha mkoani Pwani

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMA wa Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum Al Shaimar Kweigyir Semeni Kingaru, anayeitwa Kibibi Haji Pembe, amefariki Dunia leo saa tano asubuhi akiwa na umri wa miaka 80.
Semeni Kingaru kulia ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir, akiwa na mama yake mzazi Bi Kibibi Haji, ambaye amefariki Dunia leo asubuhi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

Mama huyo amefariki nyumbani kwake kijiji cha Misugusugu,wilayani Kibaha, mkoani Pwani, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mtoto wa marehemu huyo Kingaru ambaye ni Katibu wa mbunge Al Shaimar aliuambia mtandao huu kuwa mama yake atazikwa kesho saa 10 jioni kijijini hapo kwa ajili ya kumsitiri.

Alisema kuwa kwa wanaopenda kushiriki kwenye msiba huo watalazimika kushuka katika kituo cha kijiji cha Misugusugu ambapo ndipo sehemu atakapozikwa marehemu mama yake.

Msiba huo wakati unatokea, Kingaru alikuwa nchini Uganda katika majukumu yake na kulazimika kusitisha shughuli hizo kwa ajili ya kuwahi msiba wa mama yake.

No comments:

Post a Comment