Pages

Pages

Wednesday, March 11, 2015

Basi la Majinja lateketeza roho za watu zaidi ya 50 Mafinga

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
MAAFA. Ajali kubwa na ya kusikitisha imetokea maeneo ya Changarawe, Mafinga kwa kuhusisha basi linaloitwa Majinja lililoangukiwa na kontena la gari ya mizigo, kufuatia kukwepa mashimo katika barabara hiyo. Basi hilo la Majinja lilikuwa linatokea mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam, ambapo zaidi ya watu 50 wanahofiwa kupoteza maisha.

Habari kutoka katia chanzo cha ajali hiyo zinasema kwamba ajali hiyo ni mbaya kiasi cha wenye roho dhaifu kushindwa kuiangalia kutokana na aina ya ajali yenyewe na jinsi ilivyoweza kupoteza roho za watu weng katika ajali hiyo.

Shuhuda aliueleza mtandao huu kwamba kontena hilo limeangukia basi hilo kiasi cha kuwapotezea maisha abiria wengi waliokuwa kwenye gari hilo. Taarifa zaidi ya ajali hiyo zinaendelea kutafutwa baada ya kupata upande wa jeshi la polisi mkoani Mbeya ambao ndio wazungumzaji wakuu.

No comments:

Post a Comment