Pages

Pages

Friday, February 20, 2015

Mradi wa NewsRadar wa ukusanyaji wa taarifa za kibiashara wazinduliwa jijini Dar es Salaam

Mshauri mkuu wa mradi wa NewsRadar, Romana Gersuni kutoka Ujerumani akielezea jinsi teknolojia hiyo mpya na ya kisasa ya ukusanyaji taarifa mbalimbali ya Push Observer inavyofanyakazi zake.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Sekta zote Nchini sasa zinaweza kupata taarifa mbali mbali zilizorushwa kwene vyombo vya habari kupitia teknolojia mpya ya usambazaji taarifa ijulikanayo kwa jina la NewsRadar ya kampuni ya Push Observer.

Push Observer Limited ni kampuni ya Tanzania inayomiliki vyombo vya kiinteligencia na teknolojia ya sanaa ya kufuatilia, kukamata na kuchuja vyombo vya habari - magazeti, matangazo (radio & televisheni), Internet na uchambuzi, ripoti ya ushindani kwa ajili ya biashara, serikali na wateja wengineo wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Mkuu wa mikakati wa kampuni ya Six Telecoms ambayo ni kampuni mama ya Push Observer, Rashid Shamte akielezea faida ambazo watazipata kampuni mbalimbali nchini, husasani za kibiashara kwa kujiunga na huduma ya NewsRadar waliyoianzisha nchii.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya Push Mobile Fred Manento akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ufanisi wa mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini.
Afisa Mawasiliano wa kampuni ya Push Observer, Tunu Makamula akiteta jambo na wadau wa kampuni hiyo waliohudhuria semina elekezi na uzinduzi rasmi wa mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini.

Hivi sasa, Push Observer wanachunguza vituo vya redio 90+, vituo vya televisheni 15+, magazeti (magazeti, majarida, magazeti na majarida) 70+ na machapisho online ikiwa ni pamoja na blogs na mitandao maudhui. Observer ni kampuni ya kiTanzania inayoongoza kidigitali, kwa viwango vya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa katika data na uanachama na vyombo kama FIBEP, Nudge, Vision Critical, na Harvard Innovation Labs.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mikakati wa Six Telecoms, Kampuni mama ya Push Observer, Rashid Shamte alisema kuwa kupitia teknologia hii ya usambazaji ya kisasa, wateja wao wataweza kupata habari taarifa muhimu na mpya masaa ishirini na nne ya wiki. Aliongeza kuwa,tumezindua teknolojia hii kwa wateja wetu kutokana na teknologia ya uchunguzi wa vyombo vya habari kubadilika sana miaka ya karibuni”.

“Huduma hii ya kusambaza taarifa imekuwa ya kisasa, rahisi na ya ubora wa hali ya juu kutokana na uwekezaji wetu katika teknolojia hii. Wana vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kupata taarifa kupitia televisheni, magazeti, mitandao ya kijamii na redio kwa muda muafaka, vifaa hivyo vinauwezo wa kupata taarifa had 350,000 kutoka vyombo mbali mbali. Kwa kutambua mahitaji ya wateja wetu kupata habari na taarifa za muhimu tumeamua kuzindua huduma hii na ili kuwahakikishia wateja wetu upatikanaji wa taarifa muhimu na taarifa zinginezo za kwene vyombo vya habari kwa muda muafaka” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Tom Kyalo.

No comments:

Post a Comment