Pages

Pages

Friday, July 04, 2014

Safari ya Humud Sopafaka yapata baraka



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIUNGO wa zamani wa Simba aliyekatisha mkataba wake Abdulhalim Humud, ataanza rasmi kuitumikia klabu yake mpya ya Sofapaka ya nchini Kenya keshokutwa, baada ya kupata hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC).

Humud ambaye kipaji chake soka kilianza kuonekana akiwa na timu ya Mtibwa ya Sugar ya Morogoro, yupo tayari kwa ajili ya kuanza rasmi maisha mapya ya kutumikia Sofapaka ya nchini Kenya, baada ya kumalizana na klabu hiyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Humud alisema amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuichezea Sofapaka, baada ya timu hiyo kuonyesha nia ya kumuhitaji  kwa muda mrefu ili kutumikia klabu hiyo nchini Kenya.

Alisema kuwa Sofapaka kwa sasa ipo katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Kenya, huku akiamini klabu hiyo itamuwekea mazingira mazuri ya kuonyesha soka la aina yake ndani ya timu hiyo.

“Mimi nashukuru mungu kwa kila jambo nimekuwa nikikutana na mitihani mingi, lakini mungu amenipa ujasiri na kuishinda sasa hivi nimesajili na Sofapaka, nimekuja kuaga kwa ajili ya kurudi nchini Kenya kuanza kuitumikia klabu yangu hii.

Msimu uliopita Humud alijiunga na Simba akitokea Azam FC, ambayo ilishindwa kutambua mchango wa kiungo huyo na kumsotesha benchi misimu miwili, kisha baadae msimu uliofuata alirudi tena kuitumikia Simba.

Hata Hivyo Humud alishindwa kupata namba katika kikosi cha Simba, tangu Kikosi hicho kiwe chini ya Kocha Mcroatia Logarusic ambaye alichukua mikoba ya kuinoa Simba kutoka kwa Wazawa Abdallah Kibaden na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio.’ 

Kutokana na mizengwe hiyo kiungo huyo aliamua kukatisha mkataba wake na Simba mara baada ya msimu wa Ligi Kuu Bara kumalizika huku timu ya Azam FC wakitawazwa kuwa mabingwa wapya.

No comments:

Post a Comment