Pages

Pages

Monday, July 07, 2014

Mikakati ya uzinduzi wa albamu ya Rose Mhando yawekwa

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua akitangaza Uzinduzi mkubwa wa Albam ya Shikilia Pindo maarufu kwa jina la FACEBOOK ya mwimbaji nguli wa muziki wa injili Rose Muhando, 

Msama alisema kuwa albamu hiyo itazinduliwa Agosti 3 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond-Jubilee jijini Dar es Salaam na baada ya hapo itatambulishwa katika mikoa kadhaa nchini.

 Msama amesema kuwa baada ya albamu hiyo kuzinduliwa jijini Dar,Rose Muhando ataitambulisha tena albamu hiyoa kwa mashabiki wake Agosti 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Amesema kuwa kwa upande wa mkoa wa Mwanza,Rose Muhando ametoa kipau mbele kwa jiji hilo kuwa chaguo lake la kwanza baada ya uzinduzi wa jijini Dar es Salaam.Msama amewataka mashabiki wa mwimbaji huyo nyota wa nyimbo za injili hapa nchini kujitokeza kwa wingi na kumuunga mkono.
Msama amesema kuwa Rose Muhando anaendelea kujipanga vyema kuhakikisha anawapa burudani ya nguvu,

Kwa mujibu wa Alex Msama amesema kuwa nyimbo zilizopo katika albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.

Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

No comments:

Post a Comment