Pages

Pages

Wednesday, July 02, 2014

Aveva kukabidhiwa ofisi Julai 8

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU ya Simba, inatarajia kumkabidhi ofisi rais mpya wa klabu hiyo, Evans Aveva, Julai nane mwaka huu, sambamba na kuanika mambo yote, ikiwamo Milioni 420 zilizotajwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Rage alitangaza kwa waandishi wa habari kuwa anaondojka madarakani huku akimuachia rais mpya Sh Milioni 420, jambo ambalo limepokewa kwa hisia tofauti na wadau na mashabiki wa soka.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kwamba kwa sasa taratibu za ofisi hiyo zinaandaliwa kwa ajili ya kumkabidhi Rais huyo ofisi kw ajili ya kuongoza baada ya kuchaguliwa kwa kishindo na wanachama wake.

Alisema kuwa anaamini pamoja na Milioni 420 zilizotajwa na mwenyekiti Rage, Simba pia ina mambo mengi ambayo kisheria lazima yaandaliwe kwa ajili ya kumpa mwanga wa utendaji wake kwa maendeleo ya klabu yao.

“Makabidhiano rasmi ya ofisi yamepangwa kufanyika Julai nane ambapo taratibu zote zitawekwa hadharani ili kuongoza kwa miaka minne baada ya kuchaguliwa na wanachama wake Juni 29.

“Kuhusu hizo Milioni 420, ni vyema pia wadau wakasubiria siku hiyo ya makabidhiano kwasababu kila kitu kitawekwa hadharani ili kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa na kuiletea maendeleo klabu yao,” alisema Kamwaga.

Aveva ndio rais wa kwanza wa klabu hiyo tangu Katiba ya Simba iliposajiliwa na kuondoa neno mwenyekiti na kutambulika kama Rais, akirithi mikoba ya Rage, huku wanachama wengi wakiwa na imani naye.

No comments:

Post a Comment