Pages

Pages

Sunday, June 22, 2014

Yanga yawakalia kooni wanafiki



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, imewataka wanachama wenye mapenzi mema na klabu yao kusikiliza habari kutoka ndani ya uongozi na sio zinazotoka kwa wanaopenda kuzalisha migogoro klabuni kwao.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kulia akiwa na Msemaji wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto katika matukio ya klabu hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kwamba mengi yanayoibuliwa na watu hao yanatokana na kuwa na malengo ya kuivuruga klabu yao.

Alisema kwamba baadhi ya watu hao wamekuwa wakiibua hoja nyepesi, ikiwamo ya mkutano wa dharula kwa ajili ya kuleta matatizo klabuni kwao, hivyo kila anayeipenda klabu hiyo anapaswa kusikiliza habari kutoka ndani ya uongozi wao na si zile zinatolewa kienyeji.

“Yote yanayofanywa ni kwa ajili ya klabu ya Yanga, hivyo nadhani kila mwenye mapenzi mema na timu hii anapaswa kuwa makini na kusikiliza maneno kutoka kwenye uongozi, ikiwamo hatua ya kujiorodhesha kwa wale wasioafiki uamuzi wa Juni Mosi mwaka huu.

“Watu hao hawana mapenzi mema na Yanga, ndio maana wanaweza pia kugomea hatua ya kuorodhesha majina, ukizingatia wanachotaka wao ni kuona klabu yetu inashindwa kuweka mipango ya kimaendeleo,” alisema.

Hatua ya kuanza kuorodhesha majina ya wanachama wasioridhishwa na kuongeza muda wa Uchaguzi Mkuu, imetangazwa juzi na mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, huku ikianza leo na kufikia tamati Jumamosi.

No comments:

Post a Comment