Pages

Pages

Thursday, June 05, 2014

Taifa Stars kuingia kambini Juni 11



KIKOSI cha Taifa Stars kinaingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.

Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.

Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.

No comments:

Post a Comment