Pages

Pages

Friday, June 13, 2014

Mkesha wa Huduma ya AFLEWO kufanyika Juni 13 katika Kanisa la City Christian Center, Upanga


Mchungaji Abel Orgenes (wa kwanza kulia) wa Kanisa la International Evangelism akiongea machache na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Anayefuatia ni Mchungaji Fred Okello wa Kanisa la Upper Room Ministries Tz, Mchungaji Deo Lubala wa Kanisa la Word Alive pamoja na mwenyeji wao Mchugaji Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste.
Mchungaji Abel Orgenes (wa kwanza kulia) wa Kanisa la International Evangelism akiendelea kufafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. 
Mchungaji Deo Lubala (katikati) wa Kanisa la Word Alive akiongea machache na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. 

Anayefuatia kulia ni Mchungaji Fred Okello wa Kanisa la Upper Room Ministries Tz na mwenyeji wao Mchugaji Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste.
Huduma ya AFLEWO imeandaa mkesha wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Waimbaji zaidi ya hamsini kutoka makanisa mbali mbali watakuwa kwenye jukwaa moja wakisifu Mungu.

 Waumini na Wachungaji na maaskofu watakusanyika kumsifu na kumuomba Mngu kwa ajili ya taifa la Tanzania hasa kwa ajili ya mchakato wa katiba na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2015.
Mkesha huu maalum utafanyika kesho Ijumaa Juni 13, 2014 katika kanisa la City Christian Center, Upanga jijini Dar es Salaam (CCC) lililoko karibu na Chuo Kikuu cha Mzumbe. Kutakuwa hakuna kiingilio, watu wote mnakaribishwa kusifu na kuabudu.

No comments:

Post a Comment