Pages

Pages

Thursday, June 05, 2014

Kigoda kuhamia Segera kuandaa mashindano ya kandanda

MASHINDANO ya mpira wa miguu yanaandaliwa Segera Handeni na kudhaminiwa na mbunge wa jimbo la Handeni Dkt Abdallah  Omari Kigoda.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti  wa CCM kata ya Segera Mohamed Twaha mashindano hayo yataanza hivi karibuni ambapo kikao cha kutengeneza ratiba na kanuni ilikuwa kifanyike leo katika kijiji cha michungwani lakini kimeahirishwa baada ya baadhi ya viongozi wa timu husika kutotokea.


Mwenyekiti huyo aliendelea kuhabarisha kuwa katika mashindano hayo mshindi wa kwanza anatarajiwa kupata 200000 za kitanzania,jozi moja ya jezi na mpira wa kisasa kabisa,mshindi wa pili nae anatajiwa kupata shillingi 100000 za kitanzania na jezi wakati mshindi wa tatu atajinyakulia shillingi 50000 za kitanzania pamoja na jezi.

Mashindano hayo yatajumuisha vijiji vyote vinavyounda Kata ya Segera ambavyo ni masatu, mailikumi, mandera, jitengeni,chan'gombe, michungwani na segera.

No comments:

Post a Comment