Pages

Pages

Sunday, May 11, 2014

Yanga yamtwisha mzigo kocha wao wa zamani, Pluijm



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KOCHA wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm aliyepata timu nchini Uarabuni amekabidhiwa jukumu la usajili wa timu hiyo baada ya yeye mkataba wake kufikia ukingoni.

 Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuph Manji alisema Hans amewahaidi kuwaletea wachezaji wazuri.  “Hans aliahidi kuleta wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga sambamba na mridhi wake, hivyo tunasubiri kutoka kwake.
 “Pia ametuhaidi kutuletea kocha mzuri lakini bado tuna haki ya kumkataa au kumkubali kwa maslahi ya timu hii,”alisema.

 Manji ambaye amedaiwa kutokuwa na nia ya kuendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, alisema kwa sasa hawana presha juu ya kupatikana wachezaji wazuri.
 Alisema wamefikia kumuani kocha huyo wa zamani wa Yanga kuwa atakuwa na nafasi nzuri ya kuwaletea wachezaji wazuri kwa ajili ya maendeleo ya timu yao.

No comments:

Post a Comment