Pages

Pages

Thursday, May 22, 2014

Miss Dar City Center hapatoshi Jumamosi, warembo bomba kuchuana vikali


Mratibu wa shindano la Miss Dar City Center, Judith Charles, akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea kwenye shindano hilo litakalofanyika Jumamosi, katika viwanja vya Dar Free Center, jijini Dar es Salaam. Waliosimama ni baadhi ya warembo watakaochuana katika tukio hilo la aina yake.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MASHABIKI wa sanaa ya urembo, keshokutwa Jumamosi ya Mei 24, watakuwa na kazi moja ya kumshuhudia mrembo wa Miss Dar City Center, shindano litakalofanyika katika viwanja vya Dar Free Center, jijini Dar es Salaam.
Tunaelewana jamani?
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Shindano hilo, Judith Charles, alisema kuwa tukio hilo litasindikizwa na burudani kadhaa, akiwamo TID na Sky Light Band.

Mazungumzo yanaendelea juu ya shindano hilo.
Alisema kuwa taratibu zote za kuelekea kwenye kilele hicho cha kumpata Miss Dar City Center zimekamilika. “Litakuwa ni shindano la aina yake ambapo mabinti wetu wapo katika hali nzuri kwa ajili ya kuonyesha shoo nzuri kwa wadau wote watakaohudhuria.

“Naomba mashabiki wa urembo na burudani nyingine waje kwa wingi katika shindano hili kujionea umahiri wa warembo na uchu wa mafanikio katika sanaa ya urembo,” alisema Judith. Katika maeneo mbalimbali ya Tanzania, mashindano ngazi ya vitongoji ya urembo yameendelea kufanyika kwa ajili ya safari ya Miss Tanzania, baadaye mwaka huu.

No comments:

Post a Comment