Pages

Pages

Saturday, May 03, 2014

Makamu wa Rais Dkt Bilal alipongeza kanisa la Methodist Tanzania



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAKAMU wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, amelipongeza Kanisa la Methodist Tanzania, chini ya uongozi wa Baba Askofu Mkuu, Dkt. Byamungu kwa hatua nzuri ya kuchangia harakati za kimaendeleo nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, baada ya kumkabidhi Katiba na Kanuni za Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kuwekwa Wakfu (kusimikwa) askofu huyo, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli dhehebu la Methodox, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014. Picha na OMR.

Akizungumza katika sherehe la kusimikwa Askofu Mteule Alen Siso, zilizofanyika Jimbo Teule la Mashariki na Pwani, jijini Dar es Salaam, Dk Bilal alisema kuwa kanisa hilo linapanuka sanjari na kuchangia mambo mengi ya kimaendeleo.

Alisema kuwa Kanisa la Methodist Tanzania, lilianza kutoa huduma ya kiroho hapa nchini, Juni 12 mwaka 1991 lakini ndani ya miaka 23 tu, limeweza kuchangia nyanja mbalimbali za maendeleo ya jamii.

“Ujenzi wa hospitali tano mkoani Geita, shule mkoani Arusha, uchimbaji visima virefu kwa shule na magereza  katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, na ujenzi wa Chuo cha Theolojia  huko Dodoma na Arusha, ni baadhi tu ya mambo mengi mema, yanayofanywa na kanisa hili. 

“Kwa niaba ya Serikali, nawapongeza  kwa kazi kubwa mnayofanya, huku nikiwataka tuendelee kuwa karibu nanyi,   kwa kila jambo mtakaloona tunapaswa kushirikiana,” alisema.

No comments:

Post a Comment