Pages

Pages

Sunday, May 25, 2014

Kiingilio cha chini Stars na Malawi Sh elfu 5,000 tu



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KIINGILIO cha chini cha mechi ya kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (Flames) itakayofanyika kesho Mei 27 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Sh. 5,000.

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.

Taarifa iliyotumwa kweenye vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni ili kutoa fursa kwa washabiki wengi kuishuhudia timu yao, licha ya kufanyika siku ya kazi.

“Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili asubuhi ya siku hiyo hiyo ya mechi kutoka Tukuyu mkoani Mbeya ambapo imepiga kambi yake chini ya Kocha Mholanzi Mart Nooij,” alisema.

Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi tayari ipo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotumiwa na timu zote kama maandalizi ya mwisho kwa ajili mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON).

Wakati Stars kwenye mechi za AFCON itarudiana na Zimbabwe jijini Harare, Flames nayo itakuwa ugenini N’djamena kukabili Chad.

No comments:

Post a Comment