Pages

Pages

Wednesday, May 21, 2014

Katibu Mkuu IRFA ajiuzulu



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA), Eliud Mvella amejiunga na Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Amejiunga na Sekretarieti ya TFF katika Idara ya Sheria na Vyama Wanachama kuanzia leo (Mei 21 mwaka huu) ambapo atashughulikia masuala ya wanachama.

Mvella alijiuzulu rasmi wadhifa wake IRFA jana (Mei 20 mwaka huu). Mwenyekiti wa IRFA, Cyprian Kwihyava amepokea barua ya kujiuzulu huko ambapo ameelezea masikitiko yake kwa uamuzi huo wa Mvella.

Ni imani ya TFF kuwa Mvella atatumia uzoefu wake wa muda mrefu katika uongozi wa mpira wa miguu kuhakikisha TFF inaimarisha uhusiano wake na wanachama wake.

TFF ina wanachama 44 ambao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

No comments:

Post a Comment