Pages

Pages

Tuesday, May 13, 2014

Extra Bongo kuvamia Handeni Ijumaa



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi Extra Bongo Next Leval wazee wa Kimbembe inatarajia kufanya onyesho maalumu la utambulisho wa albamu yao mpya ya ‘Mtenda Akitendewa’ kwa wakazi wa Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga keshokutwa.

Kaimu Meneja wa bendi hiyo Juma Kasesa, alisema kuwa ni muda mrefu hawajatoa burudani mkoani Tanga , hivyo umefika wakati wao kutambulishwa rasmi nyimbo zao mpya zilizopo katika albamu hiyo.

Albamu hiyo imebeba jumla ya nyimbo sita ambazo ni Mama Shuu, Ufisadi wa Mapenzi, Falsafa ya maisha, Bakutuka Mgeni pamoja wimbo uliobeba jina la albamu Mtendwa Akitendewa.

Alisema baada ya uzinduzi  huo watawatambulisha wanamuziki wao wapya rapa Steven Sauti ya ng’ombe  na Alice waliyemchukua kutoka kituo cha kukuza vipaji Tanzania (THT) katika kuhakikisha bendi yao inafanya kazi vizuri.

“Tuliwaahidi wakazi wa mji wa Tanga kuja kuzindua albamu yetu kwao , hivyo tutakwenda kukamilisha ahadi yetu pamoja na kuwatambulisha wanamuziki wetu wapya ambao watapanda jukwaaji kwa mara ya kwanza,”alisema.

Alifafanunua baada ya onyesho hilo watarejea jijini Dar es Salam ambapo Jumamosi watakuwa kwenye uwanja wao nyumbani Meeda Club huku Jumapili wakiendelea na Bonanza la Njia ya Panda ya Kunduchi.

No comments:

Post a Comment