Pages

Pages

Tuesday, May 20, 2014

Chokoraa ajiandaa kuzichapa na Abdul Manyenza Manzese

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MWANAMUZIKI na kiongozi wa bendi ya Mapacha watatu Khalid Chokoraa, anategemea kupanda ulingoni Jumamosi ya Juni 24 katika Ukumbi wa Friends Corner  kuzipiga na bondia chipukizi mwenye uchu wa ushindi  muda wote awpo ulingoni, Abdul Manyenza. 
Chokoraa kushoto akijifua vilivyo kwa pambano hilo.
Chokoraa alisema muda mrefu amekuwa akifanya mazoezi ya  kujenga mwili na ya ngumi kwa muda mrefu na amekuwa akipigana na mabondia tofauti tofauti mazoezini na kuona uwezo wao ni wa kawaida, hivyo anataka kuwaonesha kama ana kipaji  kingine zaidi ya kumba muziki wa dansi.

Alisema amekuwa akijifua katika gym ya Bigright Boxing ya Mwananyamala  chini ya mwalimu wake bondia  mkongwe Omar Athuman ‘Van Dame’ kwa lengo la kumsambaratisha mpinzani wake.

Siku hiyo kutakuwa na mapambano ya ubingwa kati ya Karama Nyilawila na Said Mbelwa wakigombea ubingwa wa UBO-AFRICA ,wakisindikizwa na kina Chokoraa na Abdul Manyenza, Suleiman Galile akimkabili Abdala Pazi ‘kiroba’ nae  bingwa wa afrika Alan kamote wataoneshana umwamba na Adam ngange, Ramadhan kumbele atazipiga na Hassan kiwale”morobest” , idd athuman na julias kisarawe, nao wababe wa majigambo Zumba kukwe wataoneshana kazi na Kamanda wa makamanda, pia kutakuwa na pambano mengine mengi tu ya utangulizi ya mabondia wa tanga watazipiga na mabondia wa dare es salaam. 

Kama vile Athuman boxa wa tanga atazipiga na waite juma wa chalinze, Rajabu mahoja wa tanga atazipiga na kaisi wa darn a mengineyo yenye kuleta hamasa na burudani za mchezo wa ngumi, kwa vijana kuonesha vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment