Pages

Pages

Saturday, May 24, 2014

Arobaini ya Muhdin Gurumo kufanyika kesho Jumapili

KESHO Jumapili ndio arobaini ya mzee Muhdin Gurumo maarufu kama Mjomba au Kamanda, baada ya kufariki siku kadhaa zilizopita. Shughuli ya arobaini ya Gurumo itaanza saa saba mchana, nyumbani kwake Mabibo External.

Marehemu Muhdin Gurumo, enzi za uhai wake, akiwa jukwaani.
Wadau wote bila kusahau mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi Tanzania, wanaombwa kufika ili kuendeleza dua kwa mzee Gurumo. Shughuli ilipaswa kufanyika leo Jumamosi, ila ilisogezwa mbele ili wadau hao wapate kushiriki pia mazishi ya marehemu Amina Ngaluma.


No comments:

Post a Comment