Pages

Pages

Thursday, April 17, 2014

Simba waipania vilivyo Yanga SC



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema kwamba wana kila sababu ya kushinda katika mechi yao dhidi ya Yanga Jumamosi ili waweke heshima kwa soka la Tanzania.
Simba jana iliondoka na kuelekea Visiwani Zanzibar walipoweka kambi yao kwa ajili ya kujiwinda na mechi ya mtani wao wa jadi, Yanga itakayopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo mchana, Katibu Mkuu Kamwaga alisema kuwa hawana wasiwasi na mechi yao na Yanga, wakiamini kuwa watajenga heshima yao kwa soka la Tanzania.
Alisema wanaamini kwa pamoja wachezaji wote watafanya kazi nzuri kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo muhimu unaosubiriwa kwa hamu na wadau wa soka hapa nchini.
“Tunajiamini kuwa matokeo mazuri ya uwanjani yatatuweka katika nafasi nzuri kushinda mbele ya Yanga, ukizingatia kuwa timu ipo vizuri na imejiweka sawa Visiwani Zanzibar.
Benchi la ufundi kwa pamoja linajua namna gani tuna kila sababu ya kushinda mbele ya Yanga, ukizingatia kuwa timu yetu imepata nafasi mbaya kiasi cha kushindwa kutwaa ubingwa wa Bara,” alisema.
Mbali na kushindwa kutwaa ubingwa wa Bara, Simba pia imeshindwa walau kushika nafasi ya pili, ikiambulia nafasi ya nne kwa kujikusanyia pointi 37 katika ligi.

No comments:

Post a Comment