Pages

Pages

Tuesday, April 22, 2014

Pitia kwa urefu tamko la UVCCM dhidi ya UKAWA

Leo Nitatumia maneno makali kidogo ili tuelewane kiurahisi. Wapinzani wa Nchi hii ni "BAPHOON". Maana ya BAPHOON ni Watu au Kundi la Watu linalotumika Kwa Maslahi ya Mataifa Mengine Kuangamiza Taifa Lao. Wako Tayari Hata Kuchukua Mabomu na kulipua Nchi yao Wenyewe. Hawa ndio wanaojiita UKAWA (THE BAPHOON)
Imani namba Tano na namba nane za Chama Cha Mapinduzi kwa pamoja zinasema:
Cheo ni Dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu na Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko.
Paul C. Makonda, Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM ambaye pia ni Mjumbe Bunge Maalum la Katiba
Kwa tafsiri ya Imani ya Chama tunakubaliana na maneno ya Mwanahistoria wa zamani wa Uingereza Lord Acton aliyewahi kusema; “Power tends to Corrupt, and absolute power corrupts absolutely. Great men are almost always bad men” Yakimaanisha kuwa; “Madaraka yana tabia ya kuwaharibu walio nayo, na wenye madaraka makubwa Zaidi huharibika Zaidi kwa kuwa hata watu wema hugeuka kuwa wabaya wakishakuwa na madaraka”

Na sisi Vijana Wazalendo tunasema; “Watu wenye Madaraka Makubwa Wakiharibiwa na hayo madaraka hulewa hayo madaraka na kuanza hata kutukana kudharau waliowapa madaraka hayo. Lakini wenye madaraka makubwa wanaojua kuwa madaraka yao ni dhamana, kwanza huwa wapore na wanyenyekevu na hubeba dhamana kubwa ambayo wao huona madaraka hayo ni Mzigo wala si zawadi.”

Wapo wanaodhani kuwa Vyama vya Upinzani vipo kwa ajili ya Maslahi ya Taifa. Wapo wanaodhani Vyama vya Upinzani ndio mkombozi wao. Na wapo wanaodhani muarobaini wa matatizo ya taifa hili ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ni vyama vya Upinzani. Ukweli halisi wamepotoka sana. Vyama vya Upinzani vipo kwa maslahi yao tu na vimekuwa ni dhaifu kiasi haviwezi kuaminiwa kupewa dhamana ya Uongozi wa Taifa hili.


Hatuna haja ya kuwaambia BAVICHA waombe radhi kwa matamshi yao yasiyo na adabu waliyoyatamka jana dhidi ya Rais wa Jamhuri na Waziri Mkuu kwa sababu tunajua wanadhani wako sahihi. Lakini tunajua wanajua hawako sahihi na wanafanya hivyo ili kuwaridhisha mabwana zao ambao wanawatumia wao kutengeneza mitaji yao kisiasa. Wao wanabaki tu kama kigenge fulani ambacho kama kikiachwa kikue na uwongo wake mwishowe kitaaminiwa na hapana shaka nchi hii ipo siku itaongozwa na Vichaa.

Tuelewe Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ndiyo Lulu pekee iliyobaki Afrika ambayo imeundwa na sisi wenyewe , kwa hiari yetu wenyewe baada ya kukomboa sehemu zake mbili kutoka katika Ukoloni. Haiwezekani tuache Muungane uchezewe tu na wachache wetu ambao kinachowasukuma ni Uroho tu wa madaraka.

Tulipoanzisha Mfumo wa Vyama vingi, tulidhamiria kuwa na vyama vyenye nguvu za dhati ambazo ama zingekuwa kubwa kuliko CCM ili kuweza kuiwajibisha serikali sawasawa nayo iwajibike moja kwa moja kwa ujenzi wa taifa. 


Miaka 21 baada ya kuwa na mfumo wa vyama vingi, tumekuwa na vyama legelege ambavyo havina dira wala mwelekeo badala yake vimejikita katika uchochezi na ulaghai. Hali hii inatupa wasiwasi kama kweli hivi ni vyama vya siasa ama ni vikundi tu vya harakati vinavyofanya siasa. 

Watanzania wako tayari kuamini Upinzani lakini si kwa miaka hii ya karibuni,ni mpaka tutakapopata vyama vyenye nia thabiti ya kuleta maendeleo ya nchi hii huku vikithibitisha kwamba vitadumisha muungano wa nchi mbili serikali mbili na kuheshimu Katiba ya Nchi.

Chama Cha Mapinduzi kinabaki Imara na Msimamo thabiti wa Kuendelea na Jamhuri Muungano wa nchi mbili na Serikali Mbili. Azimio la kutaka serikali tatu si mara ya kwanza sasa. Azimio kama hili lilikuwepo Mwaka 1993 kwa hoja Binafsi ya Wabunge 55 (G55) iliyopelekwa na Mh. Njelu Kasaka Mbunge wa Chunya.

Kwa kikao Cha Bunge cha August 24-27, Bunge liliridhia mchakato wa kuanzisha serikali ya Tanganyika. Lakini kwa Uthabiti wa CCM ambao ni imara sana sasa kuliko mwaka 1993, kilisimamia mfumo wa kubaki na Muungano wa Nchi mbili na Serikali Mbili. 

Msimamo wa CCM wa Mwaka 1993 ni thabiti sana sasa, hatuwezi kufufua Tanganyika isipokuwa tutatumia mfumo uliopo kutatua kero za Muungano zilizopo. Changamoto kubwa zinazotukabili ni za kiuchumi kuliko zilivyo za kijamii na muungano wetu sana una nia thabiti ya kijamii kuliko uchumi.

Demokrasia imechukua njia hadi sasa hata mifumo ya demokrasia imeanza kupuuzwa. Nasema inapuuzwa kwa sababu hata Vichaa sasa wanaweza kuamka tu na kutoa matamko yasiyo na kichwa wala Miguu. BAVICHA ni Vijana wadogo sana ambao hawawezi kuamka na kutoa matamko waliyoyatoa ila kwa kutumwa na Bwana zao. 

Na hao Bwana zao wanafadhiliwa na Mataifa ya nje ambay hayataki kuona siku moja AFrika inaungana na kuwa taifa moja kubwa. Namna pekee ya kufanikisha uovu huo mkubwa dhidi ya Afrika, ni kuibomoa Tanzania, na wenzetu hawa wapinzani wamekubali kutumika kama vibaraka wa kudidimiza Afrika.

Hatuoni Sababu ya Kukaa Kimya, Sitanyamaza kufumbia macho Ujinga huu. Nani kawatuma BAVICHA kutoa Matamko dhidi ya Rais na Waziri Mkuu? Nani kawadanganya kuwa eti Mchakato wanaoutaka UKAWA ndio Mchakato wanaoutaka Wananchi?

Unamsikiliza Mh. Lipumba, amejawa maneno kinywani mwake ya uchochezi tu wa kidini na ubaguzi wa wazi kabisa. Hizo zote ni hila ambazo kama zisipodhibitiwa kwa kuelezwa ukweli wake kama hivi, taifa litaangamia. Tumedhamiria kupambana na hili, hatutakaa kimya Mpaka watanzania watuelewe na wawapuuze wapinzani kwa lugha zao za uchochezi.

Kwa Nini wakatake kufanyia Mkutano Zanzibar kibanda Maiti na Si Dodoma maana wote walikuwepo hapa? Hivi wapi ni Karibu, Iramba kwa Tundu Lisu au Zanzibar (Unguja Kibanda Maiti)? kuna Umbali gani Hai kwa Mbowe au Tabora kwa Lipumba au Vunjo kwa Mbatia ukilinganisha na Zanzibar? Hawa waheshimiwa wasitake kulaghai Umma, kuna ajenda wameibeba ambayo hawataki kuisema. Warudi Bungeni waje wajenge hoja maana Katiba haitapatikana Majukwaani bali kwa kukamilisha Mchakato Bungeni na ndicho CCM tutakachofanya. Tunaendelea na Bunge na tunakamilisha Mchakato hata wasiporudi.

Ikiwa wao ni vyama vya kidemokrasia na nia yao ni kujenga demokrasia, kwa nini hawataki kukaa meza ya Mazungumzo? kwa nini wakimbie mkutano halali wa kidemokrasia wasikae hapo wajenge hoja hapo badala yake wanakimbilia eti kwenye mikutano ya hadhara? 

Hapo kuna walakini na demokrasia wanayohubiri. Anayehubiri demokrasia lazima awe wa kwanza kukaa meza ya mazungumzo. Mumewasikia wakitoa matamko kwamba hawako tayari kukaa meza ya mazungumzo na serikali wala CCM, hawa ni washari na wanatangaza shari na kisha wanatafuta huruma ya wananchi. Hiyo siyo demokrasia ni Vurugu. Uhuru bila mipaka i vurugu na Demokrasia bila Utaratibu nayo ni vurugu.

Tunazo tetesi kuwa hivi vyama vinafadhiliwa na wasiotaka kuiona Afrika ikiungana na kuwa jumuiya moja kubwa yenye nguvu. wanatafuta ucku na Mchana kuisambaratisha Afrika na namna pekee ye kuisambaratisha Afrika ni kuisambarataisha Tanzania kwa maana Tanzania ndiyo kinara wa Umoja wa Afrika. Kutumiwa kwao na Ukibaraka wao uendelee lakini tuko imara sana kulinda Muungano wetu. Hawa ni BAPHOON.

Lugha za kichochezi za wapinzani wananchi wamezisikia. Wamemsikia Prof. Ibrahim Lipumba akiweka matabaka ya watu kwa sababu za Kidini, wamemsikia Tundu Lisu akipandikiza chuki dhidi ya Mwalimu Nyerere na waasisi wa Muungano, Mumewasikia viongozi wa CUF, NCCR Mageuzi, wakifanya juhudi za kufitinisha watanzania kwa kauli zao ovu. Ufitini wa aina yoyote, uwe wa kidini, kikanda, kikabila au haiba ya watu hauna budi kupigwa vita kubwa na kila Mtanzania mpenda amani.

Wakumbuke, Chuki wanazozijenga sasa, itafika mahali zitakomaa na zikishakomaa zitaanza kuwa mwiba mkali kwao wao wenyewe. Kwa maana wakifanikiwa kupanda mbegu ya chuki miongoni mwa watanzania kwa namna yoyote ile, hakuna namna ambayo hao waliowapandikiza chuki watawapenda wao. Chuki yao itawala wao wenyewe na itaangamiza taifa. Hatuwezi kuacha hili litokee tukiangalia kwa macho yetu.

Taifa halitajengwa na watu waoga wala waongo na wafitini. Watanzania wenzangu tujikite katika kujenga uchumi na kujiletea maendeleo kwani tukiendelea kuwasikiliza "BAPHOON" hawa na kuacha shughuli zetu za kiuchumi, ni kujipotezea fursa tulizo nazo kwa faida ya wengine. Hawa wanawasumbua nyie mwasikilize, wao shughuli zao za NIGHT CLUBS, GUEST HOUSE ZAO, BAR ZAO, CASINO ZAO, DALADALA ZAO, MAHOTEL, na BIASHARA ZAO NYINGINE zinaendelea kuwaingizia Pesa na wanachofanya ni kuwajaza matumaini ya uwongo huku wao wanajaa MAPESA. Kwa kuwa wameamua kutumika na mataifa ya nje kuhujumu nchi yao, bado wanalipwa kwa kazi yao ya UFITINI. Mapato yao hayayumbi na wala hayatayumba.
Ewe Mtanzania Mwenzangu, Shtuka, Achana na BAPHOON.
Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda
Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM
Mjumbe Bunge Maalum la Katiba

No comments:

Post a Comment