Pages

Pages

Saturday, April 19, 2014

23 waitwa kuungana na nyota 16 wa Taifa Stars



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam). Mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).

Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).

Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).

Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian (Mbeya).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.

No comments:

Post a Comment