Pages

Pages

Saturday, March 01, 2014

Yanga yaitungua Al Ahly Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC, leo wameanza vizuri kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Al Ahly ya Misri, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mashabiki lukuki wa kandanda.

Bao pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 82 na Nadir Haroub Cannavaro aliyetumia mbinu nzuri za kukwamisha mpira kimiani na kuwapa raha mashabiki wao. Kwa kushinda bao pekee uwanjani katika mechi ya leo, Yanga inatakiwa kuzuia sare au kushinda tena katika mechi itakayopigwa wiki mbili zijazo nchini Misri.

Hata hivyo mchezo huo wa marudiano utakuwa mgumu kutokana na histoa za timu za Misri zinavyoweza kusaka ushindi kwa hali yoyote ile. 

No comments:

Post a Comment