Pages

Pages

Sunday, March 16, 2014

Yanga wanusurika katika ajali mkoani Morogoro

BASI la Yanga lenye namba za usajili T916 CCS, limenusurika kupinduka maeneo ya Mikese, mkoani Morogoro, ikitokea huko kucheza mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mechi hiyo iliyopigwa jana, timu hizo zilichoshana nguvu, licha ya kutambiana kwa siku kadhaa katika kuelekea kwenye mechi hiyo ya aina yake na iliyohudhuriwa na watu wengi.

Katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi, wachezaji na wote waliokuwapo kwenye basi hilo walitokea madirishani, akiwamo kocha wao Mholanzi Hans van der Pluijm.

Ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo linajaribu kukwepa basi la abiria, hivyo kuingia mtaroni na kuzua hofu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile, alishindwa kuthibitisha kwa ajali hiyo baada ya simu yake kushindwa kupokewa licha ya kupigiwa simu mara kadhaa na mwandishi wa habari hizi.

Hata hivyo, hakuna aliyeumia na timu imeendelea na safari ya kurejea Dar es Salaam, licha ya kuzua hofu kadhaa kutoka kwa wadau wa soka.

No comments:

Post a Comment