Pages

Pages

Sunday, March 23, 2014

Soka la vijana lapigiwa chapuo wilayani Handeni, mkoani Tanga



Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
KATIBU wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 ya Lyons Sport ya kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Sadiki Mbwana, amesema kwa kuwekeza kwenye soka la vijana, mpira wa Tanzania unaweza kupiga hatua kubwa.
Sadiki Mbwana, pichani.
Akizungumza mjini humo, Mbwana alisema kuwa jambo hilo limewafanya waendelee kuweka mikakati ya kuiendeleza timu hiyo ya vijana, inayotokea katika mgongo wa timu kubwa ya Men Stone.

Alisema kuwa kwa kulifanyia kazi jambo hilo, wanaamini mchakato huo utakuwa na mashiko, hivyo wanaendelea na mikakati yao kuliboresha kwa kuiunda timu hiyo vizuri.

“Naamini huu ni mpango mzuri ambao kwetu sisi utakuwa na mafanikio makubwa, jambo linalotupa moyo zaidi.

Timu za vijana zianzishwe katika kila mahala, tukiwamo sisi tunaopatikana katika wilaya, ukizingatia kuwa ndio sera yenye tija kwa soka la Tanzania,” alisema.

Kwa mujibu wa Mbwana, wanaamini kwa kuiendeleza zaidi timu yao ya vijana, wanaweza kukuza soka la wilaya yao ya Handeni na Tanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment