Pages

Pages

Sunday, March 02, 2014

Recho aahidi makamuzi makubwa kisanaa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Winfirda Josephat (Recho), mwishoni mwa wiki alifurahia siku yake ya kuzaliwa, huku akiahidi kufanya kazi nzuri zaidi kwa ajili ya kuonyesha makali yao kisanaa.
Recho akiwa na Linah
Sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa mwanadada huyo ilifanyika katika Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wasanii wenzake.

Akizungumza jijini Dar Dar es Salaam, Recho alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpa kipaji kiasi cha kukitumikia kwa mafanikio.

“Haya ni mambo mazuri kwangu kwa kuonyesha kuwa sauti yangu inavuma ndani na nje ya nchi kwa kukitumikia vyema kipaji change.

“Nitaendelea kufanya kazi nzuri ili niwape raha mashabiki wangu, hivyo wakati huu ninaposherehekea siku ya kutimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwangu, sina cha kuahidi isipokuwa kazi nzuri,” alisema.

Recho ni miongoni mwa wasanii mahiri wanaotokea katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji Tanzania House of Talents (THT), ikiwa chini ya Ruge Mutahaba.

No comments:

Post a Comment