Pages

Pages

Tuesday, March 25, 2014

Maoni kuelekea pambano la Kaseba na Mashali

Hivi karibuni watakutanishwa miamba miwili ulingoni wote wakiwa na nywele zilizotengenezwa kwa mtindo wa rasta, 
Miamba hiyo  ambayo mara nyingi huwa ndio gumzo la watu mitaani hususani wapenda mchezo wa ngumi kwa tabia zao na vibwekwa vyao  kwa raia wa kawaida, hao si wengine bali ni Japhet Kaseba na bondia mtukutu Thomas Mashali, pichani, Jumamosi ya Machi 29 katika Ukumbi  PTA, Sabasaba.

Kwa Mfano - bondia Thomas  mashali “samba asiyefugika – kama anavojiita” alizaliwa Sept 1989 na kukulia mitaa ya manzese jijini dare s salaam,akiwa mtoto mtundu,mkorofi,mgomvimgovi  na mpenda michezo kama ilivyo kwa mdogo wake Charles mashali ambaye na yeye pia  alikuwa  bondia mzuri aliyetokea kuwashinda na  kuwasumbua mabondia wengi kama kina Francis Miyeyusho na alishawahi kuchukua Ubingwa wa Taifa kabla ya kuachana na mchezo wa ngumi kwa kuumia bega.
Alishindwa kuendelea na mchezo wa ngumi na kumuachia Thomas mashali ambae ni mkubwa kwa Charles mashali aliyeanza mchezo wa  ngumi akiwa mdogo na kupigana mapambano  katika kumbi za colin na manyala park  za manzese na hapo udogoni amewahi kucheza na kina Ramadhan miyeuyusho,
Raston Phili ‘moto wa tipa’ na  marehemu papa upanga na kuwa kivutio cha wengi  ulingoni na kero kwa wengine uraiani kwa tabia yake ya kuwapigapiga  watu na kuwaonea wasio na hatia na kuendekeza ubabe usio na maana akiwa kama tembo wa mitaa ya manzese kwa tabia yake  hiyo kulimfanya awe anakwenda jela  mara kwa mara na kumpotezea dira imara katika masumbwi  na kukaa muda mrefu bila kupigana mpaka pale kuna wakati ametoka jela na kurudi tena gym kama ilivyo kawaida yake kiasili anapenda sana mazoezi na michezo alikuwa akijifua kuuweka mwili wake fiti.

Mwaka 2009 alipotokea jamaa mmoja anayeitwa juma shumbili ambae ni promota wa mapambano madogomadogo ya mchangani lakini kwa wakati huu alikuwa anaandaa zaidi katika ukumbi wa texas hall manzese na kumuandalia pambano Thomas mashali akiwa kama mbabe wa Manzese na Amadu Mwalimu akiwa kama  mbabe wa Tandika.
Matokeo yake  Mashali aliibuka mshindi  wa pambano hilo kwa kumpiga Mwalimu kwa nokauti ya raundi ya tatu na hili ndilo pambano lake la kwanza rasmi la kulipwa  na kumuingiza katika rekodi ya mabondia  wa kulipwa nchini na kumfanya watu wahamasike zaidi kutaka kumuona katika mapambano mengine akikutana na wababe wenzake.
Hatimaye alikutana na Yasin Abdallah ‘ustadh’ Rais wa Oganaizesheni wa Ngumi za kulipwa Tanzania na kumsihi Mashali aachane na mambo ya kihuni atulie katika mchezo wa ngumi, kwani ana kipaji nao.
Ustadh alijitahidi  kumtafutia mapromota na kucheza mapambano mbalimbali na mabondia wakali na kuwashinda, hatimae april 2012 alikutanishwa na seleman galile kugombania ubingwa wa taifa wa TPBO ambao alishinda mchezo huo kwa point na kuuchukua ubingwa huo tabu sana katika pambano gumu,ubingwa  ambao bado anaushikilia mpaka hii leo. 
Na baadae alipata mapambano ya kimataifa na kuwashinda mabondia wengi wa nje hususani Kenya na Uganda na kutwaa ubingwa wa Africa mashariki na kati kwa kumchapa medy sebyala wauganda, akiendeleza wimbi lake la ushindi Thomas mashali “mzee wa ghetto au simba asiye fugika – kama anavyojiita” viongozi na  wadau wa ngumi wakamkubali na kumuona ameivaa kimchezo wa ngumi, wakaona huu ni muda muafaka wa mashali kumvaa Francis cheka akiwa kama challenger anayeutaka ubingwa wa cheka, mwaka may 2013 akapoteza mchezo huo dhidi ya cheka ambao uliokuwa mkali sana kwa kukata upepo raundi ya nane na kupigwa mwishoni wa raundi ya kumi,mashali alionesha upinzani mkali kwa cheka, akiwa anajiuliza kapigwaje na cheka  alipata bahati nyingine ya kukutanishwa na bondia wa hapa nchini Mada Maugo na kugombania ubingwa wa Afika wa WBFed (world boxing federation) na kuibuka kidedea baada ya kumpiga Mada Maugo kwa point, na kutwaa ubingwa huo afrika akachaguliwa kwenda urusi kugombania ubingwa wa mabara dhidi ya arif magomedov  huko alipata kipigo kikali toka kwa bondia huyo wa urusi katika raundi za mwazomwanzo  na kurudi nchini mikono mitupu.
Mashali kwa Kupoteza mchezo wake na  mrusi hakujaathiri  ubingwa wake wa afrika jambo ambalo viongozi wa ngumi wakiongozwa na Ibrahim kamwe walikaa na mapromota  wakaonelea huyu bwana anaweza kuzipiga na bondia wa mbeya Karama nyilawila ambao walishawahi kuzipiga zamani mwaka 2009  na pambano kutolewa sare, wakati linapangwa pambano hilo la karama na mashali  la marudiano, tayari kampuni  ya bigright promotion ilishaanza maongezi  ya kuwapiganisha mabondia  karama nyilawila na jafet kaseba, akajitokeza promota maarufu wa jijini  Tanga Ally mwanzoa  na kuwa yupo tayari kuwapambanisha mabondia hao wote katika mapambano ya ubingwa .hapo ndio mwakilishi wa UBO(universal boxing organization) nchini bw emmanuel mlundwa ambae pia ni rahisi wa PST( pugilistics syndicates of Tanzania) akasema mashali ana nafasi ya kupigana Japhet kaseba katika ubingwa huo ulio wazi katika uzani wa kilogram 79.mipango ya pambano hilo ikaanza kwa kuwakutanisha Thomas mashali na
Japhet Kaseba aliyezaliwa Decemba 1979 (miaka 10 zaid ya mashali) ambae ni Bingwa asiyepingika hapa nchini kwa kukosa bondia wakupigana nae baada ya kuwapiga mabondia wote  katika mchezo wa mateke (kickboxing) ambae pia amewahi kuwa bingwa wa Dunia katika mchezo  huo wa ngumi na mateke (kickboxing)  kwa kushinda ubingwa wa mabara nchini Holand na kuutetea nchini Japan, na baadae kugombea ubingwa huo wa Dunia dhidi ya bondia toka Ufilipino Ricky Agayas na kumpiga kwa ko ya raundi ya tatu na kutwaa ubingwa huo. Kaseba amekaa kwa muda bila kupata nafasi ya kuutetea ubingwa wake huo kwa kukosa wadhamini na hapo alipoamua kubadili aina ya mapigano na kurudi katika ngumi mchezo ambao aliucheza zamani kabla ya kickboxing. 
Alipoingia tena katika ngumi alipata nafasi ya kupigana na bingwa wa ngumi wa hapa francis cheka katika pambano la kuwakutanisha bingwa wa mateke na bingwa wa ngumi matokeo yake kaseba alishindwa na cheka na kutoridhika na matokeo hayo kwa kisingizio cha fujo zilizotokea katika mchezo huo na akawa anatafuta marudiano kwa hali yoyote ile na kumfanya abakie katika ngumi akisubiri nafasi nyingine ya marudiano na cheka akapigana mapambano yake  ya ngumi kwa kusuasua na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa taifa wa PST  kwa kumpiga maneno osward  ubingwa ambao anaoushukilia mpaka leo. 
Kaseba alicheza nchi Australia akigombea ubingwa nchini humo  na kupoteza. Katika pambano lililoandaliwa hivi karibuni  kati ya wababe waliopoteza ughaibuni, ikiwa na maana Japhet kapigwa Ausralia na mashali kapigwa rusia pindi japhet alijisafisha kidogo kwa kucheza na Alibaba Ramadhan wa Arusha na kumpiga kwa tabu, jambo ambalo linampa imani Mashali huwenda akamshinda Kaseba.
Marasta hao ni Japhet kaseba na Thomas Mashali ambao wanaotegemea
upanda ulingoni tarehe 29 March 2014  katika Ukumbi wa PTA Hall kugombania ubingwa ulio wazi wa Universal Boxing Organization-UBO na  mshindi katika pambano hilo atacheza na Karama Nyilawila Mei Mosi. Limeingia katika sura mpya ya wadau wengi wa ngumi kuwekeana  pesa kama kamari ya kuwa nani atashinda, tayari amejitokeza msanii Dotnata (ambae ni mshabiki mkubwa wa Kaseba) kaahidi kutoa gari endapo Kaseba atashinda. Pia kuna mdau mwingine ameahidi kutoa pikipiki kwa mshindi kati ya Kaseba na mashali siku hiyo katika ukumbi wa Karume zamani PTA hall sabasaba ambapo kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi yakiwemo pia ya ubingwa wakati katika pambano la raundi kumi Fredy Sayuni wa keko atazipiga na Rajabu Mahoja wa Tanga ubingwa wa Taifa, Alan Kamote wa Tanga bingwa wa Afrika Light Weght aliyekuwa azipige na Fadhili Awadh (aliyefariki ghafla kwa maleria)  katika pambano la Ubingwa la UBO International sasa atazipiga na bingwa wa taifa katika uzani huo bondia toka Tanga Said Mundi, nae Juma Fundi atazipiga na mkongwe Haji Juma huku Dogo anayechipukia kwa kasi Issa Omari Nampepeche wa Dar es Salaam, akizipiga na bingwa wa taifa bantam Zuberi Kitandula toka Kilimanjaro pia kutakuwepo na pambano la mabondia wakongwe wa zamani amabao sasa hivi ni walimu na marefa wa mchezo huo Said Chaku(52) atazipiga na Jocky Hamisi(58), pia Bakari Dunda atazipiga na Baina Mazola

No comments:

Post a Comment