Pages

Pages

Tuesday, February 25, 2014

Wakulima wilayani Handeni waaswa kulima mazao ya biashara na chakula



Na Mwandishi Wetu, Handeni

WANANCHI wilayani Handeni, mkoani Tanga, wameaswa kulima maza ya biashara na chakula ili kuwaondolea balaa la njaa linalowakumba kila mwaka kutokana na kutegemea kilimo cha aina moja, yakiwamo mahindi.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Muhingo Rweyemamu katika mahojiano maalum wilaya Handeni mkoani Tanga, ikiwa ni sera na mipango kabambe ya kuweka sawa jambo hilo kwa maendeleo ya wananchi wa Handeni na Tanzania kwa ujumla.


DC Muhingo alisema kuwa wakazi wengi wa Handeni wanategemea kilimo cha mahindi kama zao la biashara na chakula, jaambo linalowafanya kila wakati watu wengi wakabiliwe na njaa na kuwafanya waishi kwa tabu wakati wote.

“Ofisi yangu inajitahidi kuwaelimisha wananchi wengi waone ipo haja sasa ya kulima mazao mengi ya biashara, ukizingatia kuwa sasa wengi wao wanategemea mahindi kama zao la chakula na baadaye huuza kwa mahitaji yao.

“Naamini yapo mazao mengi ambayo endapo yatalimwa kwa wingi, mahindi yatahifadhiwa kwa ajili ya chakula wao na familia zao, maana suala la njaa Handeni linatokea kwasababu kuna mapungufu mengi, hasa ya chakula kuwa haba,” alisema.

Kwa mujibu wa Muhingo, elimu ya ziada kwa wananchi na wakulima wote kwa ujumla inahitajika wilayani humo ili watu wazoee kulima mazao mbalimbali, ukiwamo ufuta, maharage na mengineyo kwa ajili ya biashara na kuweka akiba ya chakula kwa zao la mahindi.

No comments:

Post a Comment