Pages

Pages

Wednesday, February 26, 2014

Twanga Pepeta kusugua kisigino Cheetoz



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi ya The African Stars, Twanga Pepeta, leo inafanya shoo ya aina yake katika Ukumbi wa Cheetoz, uliopo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani, alisema kuwa onyesho hilo litakuwa la aina yake, kutokana na mikakati yao.
Alisema kuwa wadau wao wataendelea kupata burudani kali kutoka kwao ili waendelee kushika usukani katika tasnia ya muziki wa dansi.
“Tumejipanga imara kuhakikisha kuwa wadau na mashabiki wetu wanapata shoo za aina yake kutoka kwetu na kuonyesha makali yetu.
“Twanga haina mpinzani na ndio bendi yenye shoo nyingi kwa wiki, ikiwamo ya Jumatano ambayo sasa tutakuwapo Cheetoz ili kufanya mambo ya maana kwenye muziki wa dansi,” alisema.
Twanga Pepeta ni miongoni mwa bendi zenye mashabiki wengi hapa nchini, huku ikijihakikishia kuwa na shoo nyingi kuanzia Jumatano hadi Jumapili.

No comments:

Post a Comment