Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Winfirda Josephat (Recho), mwishoni
mwa wiki alifurahia siku yake ya kuzaliwa, huku akiahidi kufanya kazi nzuri
zaidi kwa ajili ya kuonyesha makali yao kisanaa.
Sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa mwanadada huyo ilifanyika katika Ukumbi wa
Business Park, Kijitonyama na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wasanii
wenzake.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Recho alisema kuwa
anamshukuru Mungu kwa kumpa kipaji kiasi cha kukitumikia kwa mafanikio.
Unamjua Recho? Huyo hapo kushoto.
Recho wa THT kushoto akishow love katika sherehe yake ya kuzaliwa mwishoni mwa wiki.
Msanii Kalala Junior akiwa amembeba msanii Recho wakati wa part yake ya kuzaliwa.
Ilikuwa ni balaa. Watu walivunja kabati. Huyo wa kushoto ni Linah na anayefuata ni Birthday girl, Recho wa Kizunguzungu kwenye sherehe yake.
Hapo sasa. Msanii Recho akiwa na Linah katika sherehe yake. Kwakweli ilikuwa ni bonge la burudani kutoka kwa wanadada hawa. Hawa wote wanatokea katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talents (THT). Swali, je ni kweli Linah ana ujauzito? Tumbo lake hilo hapo linaonekana hadharani kabisa.
“Haya ni mambo mazuri kwangu kwa kuonyesha kuwa sauti yangu inavuma ndani
na nje ya nchi kwa kukitumikia vyema kipaji change.
“Nitaendelea kufanya kazi nzuri ili niwape raha mashabiki wangu, hivyo
wakati huu ninaposherehekea siku ya kutimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa
kwangu, sina cha kuahidi isipokuwa kazi nzuri,” alisema.
Recho ni miongoni mwa wasanii mahiri wanaotokea katika taasisi ya kukuza
na kulea vipaji Tanzania House of Talents (THT), ikiwa chini ya Ruge Mutahaba.
No comments:
Post a Comment