Pages

Pages

Friday, February 21, 2014

Wilaya Kilindi yapania kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji

Na Mwandishi Wetu, Kilindi

MKUU wa Wilaya Kilindi, Seleman Liwowa, amesema kwamba juhudi za kukomesha migogoro inayoweza kuichafua amani kwenye wilaya hiyo mkoani Tanga, inawekwa kwa kuhakikisha inawaweka sawa wakulima na wafugaji.
Mkuu wa wilaya Kilindi, Selemani Liwowa, pichani.
DC Liwowa aliuambia mtandao huu wa Handeni Kwetu kuwa miongoni mwa migogoro hiyo tishio inasababishwa na wakulima na wafugaji, sanjari na ongezeko la watu wilayani humo na Tanzania kwa ujumla.



Alisema kuwa ofisi yake kwa siku kadhaa sasa imejaribu kukaa na kuliangalia kwa kirefu suala hilo, hivyo anaamini watalipatia ufumbuzi kwa manufaa ya Kilindi na Tanzania kwa ujumla.


“Tumegundua kuwa migogoro hii inasababishwa na wakulima na wafugaji, huku chanzo pia kikiwa ni ongezeko la watu huku ardhi ikiwa haijapimwa.


“Nadhani tumekaa na kuona tupitie upya matumizi ya ardhi kwa upande wa wakulima na wale wafugaji ili kuhakikisha kuwa utulivu unakuwapo wilayani hapa,” alisema.


Kilindi inatokea ubavuni mwa wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, ambapo kwa sasa inaongozwa na DC wake Muhingo Rweyemamu, ndani ya Mkoa wa Tanga, ambapo p/ia upo chini ya Chiku Gallawa.

No comments:

Post a Comment