Pages

Pages

Friday, February 21, 2014

Mkwassa kurejea leo na mbinu za kuwadunda Al Ahly



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA msaidizi wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwassa, anatarajia kuwasili leo akitokea nchini Misri, akiwa na mipango kabambe ya kuwaangamiza wapinzani wao, timu ya Al Ahly.
Kocha msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwassa, pichani.

Mkwassa anarejea Tanzania, akitokea nchini humo kuwasoma Al Ahly, ambayo wataavana nayo Februari 28 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa mzunguuko wa pili baada ya kuwaondosha Komorozine, ya Comoro kwa bao 12-2.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kwamba timu yao ipo vizuri kuelekea kwenye mechi hiyo ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku wakikutana na timu ngumu.

Alisema jambo hilo liliwafanya wajipange imara, ikiwapo kumtuma Mkwassa kwenda Misri kufuatilia nyendo za Al Ahly kabla ya kukutana nao uwanjani.

“Mkwassa amepewa jukumu la kuiangamiza Al Ahly ya Misri, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo tunaamini baada ya kurejea kesho (leo), benchi la ufundi litajua wapi kwa kuanzia.

“Tunaomba tuwe na uvumilivu kwakuwa watu wote tuna shauku ya kuona Yanga inasonga mbele katika michuano ya Kimataifa, maana ndio dhamira yetu,” alisema Kizuguto.

Yanga ndio timu pekee ya Tanzania Bara ambayo inaendelea na michuano ya Kimataifa, baada ya kuifungasha virago timu kibonde ya Comoro kwa bao 12-2.



No comments:

Post a Comment