Pages

Pages

Saturday, February 08, 2014

Milioni 500 zahitajika kuokoa tiketi za elektroniki



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ILI mradi wa tiketi za elektroniki zinazotolewa chini ya uzabuni wa Benki ya CRDB, zinahitajika jumla ya Sh Milioni 500 kwa ajili ya kutoa elimu na mtangazo kwa wadau wa michezo wasiofamu utaratibu huo ulioanza kwa mara ya kwanza hapa Tanzania.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kutumika katika matumizi mbalimbali, yakiwamo matangazo na utoaji elimu kwa wadau wa soka juu ya teknolojia hiyo mpya, ambayo imelazimika kusitishwa kwa muda usiojulikana.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia siku 100 tangu aliposhinda urais wa TFFF, Jamal Malinzi, alisema kuwa mradi huo ni mpya na una changamoto nyingi zinazohitaji kufanyiwa kazi.

Alisema kuwa mkataba na wazabuni wao, benki ya CRDB unaeleza juu ya masuala ya utoaji wa elimu ya teknolojia huyo kutolewa na TFF.
“Tuna mpango wa kuendelea kukaa na CRDB juu ya kuangalia namna ya kuboresha mradi huu, maana ili ukaamilike unahitajika Milioni 500.

“Hizo ni baadhi ya changamoto ambazo mimi kama rais wa TFF, nikaamua kusitisha matumizi ya tiketi hizo hadi tutakapotangaza tena,” alisema Malinzi.
Pamoja na mambo mengine, Malinzi alitumia nafasi hiyo kuelezea mikakati kabambe ya kuhakikisha soka la Tanzania linapiga hatua, ikiwa ni kuonyesha imani ya kuchaguliwa na kupewa nafasi hiyo ya urais wa Shirikisho hilo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment