Pages

Pages

Sunday, February 23, 2014

Jay Msangi aipigia magoti serikali



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
PROMOTA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Jay Msangi, ameiomba serikali kuliangalia upya suala la kusimamishwa kwake kuandaa mapambano ya ngumi kwakuwa hali hiyo inaweza kuzorotesha mchezo huo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msangi alisema kuwa kusimamishwa kwake kuandaa mapambano ya masumbwi kumelenga kumkomoa na si kuleta chachu ya kuutangaza zaidi mchezo huo.

Alisema miongoni mwa tuhuma kuwa anadaiwa na bondia wa Marekani, Phil Williams zilishamalizika kwa kulitatua suala hilo kwa makubaliano ya bondia huyo na waandaaji wa pambano hilo lililomkutanisha na Mtanzania Francis Cheka.

“Kuna mambo mengi yanaweza kutokea nyuma ya pazia, hivyo ninachoitaka serikali ni kuangalia zaidi athari zinazoweza kutokea juu ya kusimamishwa kwangu.

“Mimi na Williams tulishamalizanaa na nipo tayari kupekeleka vielelezo juu ya bondia huyo, hivyo siamini kama harakati hizi zinaweza kuleta tija katika masumbwi,” alisema.

Mgogoro wa promota huyo umekuja wakati wadau hao wa masumbwi walishafanya mkutano wa kujadili jinsi ya kuutangaza na kuukuza mchezo wa masumbwi unaosua sua, hivyo kuonyesha kuwa bado juhudi madhubuti zinahitajika ili kukomboa ngumi.

No comments:

Post a Comment