Pages

Pages

Saturday, January 11, 2014

Wilaya ya Handeni yapitisha Bajeti ya Bilioni 7.9 kwa mwaka wa fedha 2014/2015


Mkuu wa Wilaya Handeni, DC Muhingo Rweyemamu
Na Rajabu Athumani, Handeni
BARAZA Madiwani la Halmashuri ya Mji Handeni limepitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka 20014/2015 ya kiasi cha shilingi 7.9 bilioni kwaajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo katika mji huo.

Akizungumza katika kikao maalum cha bajeti kilichofanyika jana katika ofisi za mji huo,kaimu mkurugezi mtendaji wa mji huo Thomas Mzinga alisema kuwa fedha hizo zitapatikana kutoka serikali kuu pamoja na vyanzo vya makusanyo ya ndani vya mapato na kuweza kusaidia kuendesha shughuli zao.

Mzinga alisema kuwa mbali za ruzuku kutoka serikalini pia wanatarajia kuongeza pato lao kutoka vyanzo vya ndani kama kukusanya kodi ya majengo ambayo inatarajiwa kuanza kukusanywa mapema kuanzia tarehe 15 mwezi huu ambapo halmashuri inatarajia kusanya shilingi milioni mia mbili kutoka katika chanzo hicho cha ndani.

Alifafanua kuwa makadirio ya mwaka huu wanarajia kukusanya kasma ya shilingi 7.2 Milioni kutoka nyanzo mbali mbali vya mapato ambavyo wataendelea kuviboresha ikiwemo kituo cha mabasi,machinjio na mnada ambavyo vinauwezo wa kuwa na pato la kutosha.la kuweza kuongeza pato la halmashuri ya mji.

Akisisitizia suala la kodi ya majengo Mkurugenzi huyo amewaomba wakazi wa Mji wa Handeni kutoa ushirikiano katika kulipa kodi hizo ambazo zitasaidia kuboresha huduma za jamii kama barabara,afya pia mashuleni katika kujenga maabara za kisasa katika shule ili kuondoa tatizo la wanafunzi kutosoma masomo ya sayansi.

Aidha aliongeza kuwa katika bajeti hiyo kuna changamoto mbali mbali ikiwemo wa kuchelewesha kwa kuingizwa fedha za ruzuku kwa wakati hali inayofanya kucheweshwa kwa kuendeleza miradi katika jamii hivyo kuiomba idara husika kuangalia hilo na kujitahidi kufikisha fedha hizo kwa wakati ili kukimbizana na muda wa miradi husika.

Diwani wa kata ya Vibaoni mjini humo Injinia Mkusa Nkondo alitoa angalizo kwa halmashauri kuwa wa wazi katika kutekeleza miradi kama walivyoleta bajeti hiyo mbele yao kwa kugawa miradi katika kata bila ya upendelea kwani maeneo yote yanahitaji maendeleo na ni lazima yafike kama ilivyokusudiwa ili wananchi wapate huduma bora.

No comments:

Post a Comment