Pages

Pages

Wednesday, January 08, 2014

Ushamba Mzigo, Thamani ya Mtu wazipa kiburi Mashujaa Bendi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Mashujaa bendi imejisifia juu ya nyimbo zao mbili za Ushamba Mzigo na Thamani ya mtu kuwa zilikuwa balaa baada ya kuzitambulisha mwaka jana na kupokewa kwa shangwe na mashabiki wao.
Mashujaa wakiwa chini ya Charles Gabriel Baba, maaurufu kama Chalz Baba, walikuwa kwenye pilika pilika kali za kuchuana na wakongwe wao, ikiwamo bendi ya The African Stars Twanga Pepeta.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa Mashujaa bendi, Martin Sospeter alisema kuwa mashabiki wao walipata nyimbo kali zenye kila dalili ya ubora kutoka kwao.
“Haya ndio mapinduzi tuliyoahidi kuwapatia mashabiki wetu baada ya kuhakikisha kuwa wanapata nyimbo nzuri kutoka kwetu kwa ajili ya kuona makali yetu.
“Nyimbo hizi zilipokewa kwa shangwe na mashabiki wetu ambapo kwa pamoja zilikuwa zikifanya vyema tangu zilipotambulishwa baada ya kuandaliwa kwa kiwango cha juu mno,” alisema.
Kwa mujibu wa Sospeter, wamejipanga mwaka huu waendeleze makali yao kwa kuhakikisha kuwa wanatoa burudani kali ili kujiweka kileleni zaidi katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.

No comments:

Post a Comment