Pages

Pages

Monday, January 13, 2014

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii aagiza kumalizwa kwa migogoro ya mipaka kwenye Hifadhi za Taifa

Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara na Dodoma wakati wa kikao  maalum cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya   Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Elaston Mbwilo akisitiza jambo wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma  na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya  Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
Sehemu wa wajumbe waliokutana katika kikao maalum cha Kamati za  Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba  la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Kutoka kulia: Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Profesa Alexander Songorwa na KatibuTawala wa  Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya  Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika  Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Waheshimiwa Wabunge Zabein Mhita na Moza Abeid kutoka Dodoma  wakati wa kikao hicho.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na wanahabari mara baada ya kikao hicho.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Serikali ameagiza kumalizwa kwa migogoro ya mipaka baina ya Hifadhi ya Tarangire, Pori la Akiba  la Mkungunero na wananchi iliyodumu kwa muda wa takribani miaka kumi  hadi sasa. Nyalandu amewataka wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi  hizo kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni  kuleta migogoro isiyo ya lazima. Mhe. Nyalandu alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na 

Usalama za mikoa ya Manayara na Dodoma wilayani Babati mkoani Manyara  zilizokutana kwa ajili ya kujadili suluhu ya migogoro hiyo. 
Aliongeza kusema kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro hiyo kwa  kuishirikisha jamii kwa upana zaidi huku akisisitiza kwamba Serikali itaendelea  kusimamia na kutekeleza Sheria ya Uhifadhi bila kumuonea mwananchi yoyote  na kwa kuzingatia haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment