Pages

Pages

Saturday, January 25, 2014

Mkunguni, Masjid kukipiga fainali leo Mikocheni


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

FAINALI ya michuano ya Mwenyekiti CUP inayoendelea Kata ya Mikocheni, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, inafanyika Jumapili ya Januari 26 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mikocheni, kwa kuwakutanisha Mkunguni na Masjid.

Mashindano hayo yalianza mwishoni mwa mwaka jana, ambapo lengo lake ni kutangaza vipaji vya mpira wa miguu hapa nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwendeshaji wa mashindano hayo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mikocheni, Suleiman Akida, alisema kwamba vijana wameonyesha shauku kubwa katika kushiriki patashika hiyo ya mwenyekiti Cup.

“Tunashukuru kuona mashindano yetu yanaelekea mwishoni ambapo timu hizi mbili zenye ubora wa hali ya juu zinawania ubingwa katika Uwanja wa Shule ya msingi Mikocheni.

“Tunaomba wadau waje kwa wingi kuangalia jinsi vijana wetu wanavyofanya kazi kubwa kutangaza vipaji vyao vya mpira wa miguu hapa nchini,” alisema Akida.

Kwa mujibu wa Akida, mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atapewa jezi na Sh 100,000, wakati mshindi wa pili atapewa jezi na Sh 50,000.

No comments:

Post a Comment